MSAFARA WA KATIBU MKUU WA CCM,NDUGU KINANA WAPOKELEWA KWA FARASI MIKOCHENI -WILAYA YA MOSHI VIJIJINI
Msafara wa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana ukipokelewa kwa farasi wakati wakiwasili katika kata ya TPC kijiji cha Mikocheni wilaya ya Moshi Vijijni mapema leo asubuhi,tayari kwa kuanza ziara ya jimbo la Moshi Vijijini mkoa wa Kilimanjaro.Ndugu Kinana alizungumza na Wananchi wa kijiji hicho na kuzisikiliza matatizo yao,hasa suala la Ardhi.Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana akiwa ameambatana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi wako mkoani Kilimanjaro katika ziara ya siku tisa ya Kusimamia,kuhimiza,Kukiimarisha na kutekeleza Ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 na ikiwemo pia kusikiliza matatizo ya wananchi
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana na ujumbe wake wakiwasili katika kijiji cha Magomeni mapema leo asubuhi,kulia ni Mbunge wa Jimbo la Moshi Vijijini Mh.Dkt.Cyril Chami.
Mkutano ukiendelea katika kijiji cha Mikocheni
Wananchi wa Mikocheni wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana alipozungumza nao mapema leo asubuhi,katika jimbo la Moshi Vijijini mkoani Kilimanjaro.
Wakazi wa kijiji cha Mikocheni wakishangilia jambo wakati Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana alipozungumza nao na kusikiliza matatizoo yao mbalimbali yakiwemo ya Ardhi.
Mwenyekiti wa Chama cha CHADEMA tawi la Mikocheni,wilaya ya Moshi Vijijini akitangaza kuhamia chama cha CCM,amapo pia alikabidhiwa kadi mpya ya CCM na kukabidhi kadi yake ya zamani kwa Ndugu Kinana.Pichani kushoto ni Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akisikiliza kwa makini.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akishiliki kupiga ngoma wakati wakipokelewa katika ukumbi wa CCM mkoa .
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana akizunguma katika Mkutano wa Halmashauri kuu ya wilaya na kikao cha jimbo,ambapo Ndugu kinana alipokea taarifa ya chama na taarifa ya utekelezaji wa Ilani
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana akizunguma katika Mkutano wa Halmashauri kuu ya wilaya na kikao cha jimbo,ambapo Ndugu kinana alipokea taarifa ya chama na taarifa ya utekelezaji wa Ilani
Comments