BULEMBO AGEUKWA NA WAJUMBE WAKE SAKATA LA KWENDA KWA LOWASSA

Mjumbe wa Baraza la Wazazi, Taifa na Mbunge wa Korogwe, Steven Ngonyani ‘Prof .Maji Marefu’ akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma hii jana juu ya tuhuma za yeye kutajwa na mmoja wa wajumbe wa baraza hilo kuwa aliratibu na kulazimisha baadhi ya wajumbe wa baraza hilo kwenda kumuona Mbunge wa Munduli na Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa. 
Naye Mbunge wa Korogwe
Vijijini, Stephen Ngonyani, alisema yeye alielezwa kuhusiana na safari hiyo na rafiki yake Vioroka Kajoko.
“Nimekuwa katika jumuiya hii
kwa miaka 15. Siko tayari kuchaguliwa kiongozi, marafiki wala maadui. Mimi siko
tayari  uomba radhi kwasababu sina kosa
nililotenda,”alisema Ngonyani. 
Alisema hajawahi kumshawishimtu wala kumlazimisha mtu kumpenda mtu anayempenda yeye.
 Jackline Ngonyani aliyejitambulisha kwa Lowassa kama ‘Maji mafupi’ na kutoa salam za shukrai kwa wana Ruvuma kwa jinsi Lowassa alivyo shiriki katika mazishi ya Capt. John Komba lakini jana aliwaambia waandishi wa habari kuwa alilazimishwa kushiriki katika msafara huo. Lakini wenzake wanasema yeye alikuwa mmoja wa waratibu.
Mjumbe wa Baraza Kuu la Wazazi mkoa wa Njombe, Evarist Lupenza,  akizungumza na waandishi wa habari juu ya safari yao kwenda kwa Lowassa. Pamoja nae ni Mwenyekiti wa Jumuia ya Wzazi mkoa wa Mwanza, Malila Lugoye.
  Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Mkoa wa Dodoma, Dk.
Damas Mukassa, akiwaonesha waandishi wa habari picha ambayo mjumbe mwenzao alisema wamelazimishwa kwewnda kwa Lowassa jinsi alivyo kula pozi na Lowassa.
*********************
VIONGOZI waliotajwa na Mwenyekiti
wa Jumuiya ya Wazazi ya CCMTaifa, Abdallah Bulembo, kuratibu safari ya baadhji
ya wajumbe wa jumuia hiyo na baraza la Wazazi Taifa kwenda kumsalimia Waziri
Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli Edward Lowassa jana wamekanusha vikali
kuhusika na uratibu wa baraza hilo.
Jana Bulembo aliwashukia wajumbe
waliokwenda nyumbani kwa Waziri Mkuu wa Zamani, Edward lowassa,na kumchakingaia
fedha na kumshawishi  agombee Urais na
kuwataka waombe radhi kutumia jina la baraza hilo na kasha kusubiri  kamati ya maadili.
Wakizungumza hii leo baadhi ya
wajumbe hao wamewataja waratibu walioongoza msafara wao kuwa ni pamoja na
Katibu wa CCM Wilaya ya Hanang, Vioroka Kajoro na Mjumbe wa baraza hilo kutoka mkoani
Ruvuma, Jackline Ngonyani na Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Mkoa wa Dodoma, Dk.
Damas Mukassa.
Mjumbe wa jumuiya hiyo kutoka
Mkoa wa Njombe, Evarist Lupenza, alisema aliyekuwa akiandika majina ya wajumbe
waliokwenda katika ziara hiyo ni Jackline Ngonyani. 
“Niliwasikia wakisema kwa Mzee
ni saa tatu, nikawauliza mnataka kwenda wapi, wakaniambia kuwa wanataka kwenda
kumsalimia Lowassa, name nikaandikisha jina kwa ajili ya kwenda huko,”alisema
Lupenza.
Nae Mwenyekiti wa Jumuia ya
Wazazi mkoa wa Mwanza, Malila Lugoye alibainisha kuwa hakuna mtu
aliyeshinikizwa katika safari hiyo na ilikuwa ni huru kuamua kwenda au kubaki.
 “Hakuna mtu aliyeshinikizwa kwenda kwa Lowassa
kila mtu alikwenda kwa mapenzi yake. Na hakuna mtu aliyetumia jina la Jumuiya
wakati tulipokwenda bali watu walijitambulisha mmoja mmoja,”alisema na kuungwa
mkono na Mwenyekiti wa jumuiya hiyo Mkoa wa Mwanza, Malila Lugoye.
Naye Mbunge wa Korogwe
Vijijini, Stephen Ngonyani, alisema yeye alielezwa kuhusiana na safari hiyo na
rafiki yake Vioroka Kajoko.
“Nimekuwa katika jumuiya hii
kwa miaka 15. Siko tayari kuchaguliwa kiongozi, marafiki wala maadui. Mimi siko
tayari  uomba radhi kwasababu sina kosa
nililotenda,”alisema Ngonyani.
Alisema hajawahi kumshawishi
mtu wala kumlazimisha mtu kumpenda mtu anayempenda yeye. 
 Dk Mukassa alisema yeye aliratibu ziara hiyo
kama mwenyeji wa mkoa wa  Dodoma ambaye
anakufahamu nyumbani kwa Lowassa.
 Alisema fedha walizotoa kwa ajili ya
kumchangia kuchukua fomu za Sh 600,000 zimetokana na mchango wao wenyewe kama
wanachama wa kikundi cha kusaidia cha wajumbe wa jumuiya hiyo.
“Fedha zile hazikutoka kwenye
jumuiya ya chama wala hakuna aliyekwenda pale kuwakilisha jumuiya na
niliwaeleza pale mliponiuliza na kila mtu alijitambulisha kama yeye,”alisema.

Comments