Monday, March 23, 2015

NHIF YATOA ELIMU KWA UMOJA WA MADEREVA TAXI WILAYA YA ILALA (UMATAWI)

  DSC_0030
Kaimu Mkurugenzi wa Mfuko wa Taifa wa bima ya afya (NHIF) ,Eugen Mikongoti, akizungumza na umoja wa madereva taxi wilaya ya Ilala (Umatawi), wapatao 380 jijini Dar es Salaam wakati wakitoa elimu kwa madereva taxi  kuhusiana na huduma za mfuko huo ili nao wawe mawakala kwa kuwashauri wenziwao kujiunga na NHIF.
DSC_0032DSC_0035
Umoja wa madereva taxi wilaya ya Ilala (Umatawi) wakifuatilia mada mbali mbali wakati semina hiyo.
DSC_0049
Viongozi kutoka NHIF wakimsikiliza kwa umakini Kaimu Mkurugenzi wa Mfuko wa Taifa wa bima ya afya (NHIF) ,Eugen Mikongoti, wakati akizungumza na Umoja wa madereva taxi wilaya ya Ilala (Umatawi)
DSC_0002
Picha ya pamoja.
……………………………………………………
Na Mwandishi wetu
MFUKO wa Taifa wa bima ya afya (NHIF) umewashauri wajasirimali wadogo wadogo kuunda vikundi kwa ajili ya kunufaika na huduma za mfuko huo wenye lengo la kurahisisha upatikanaji wa huduma ya afya kwa urahisi ndani ya jamii.
Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi wa mfuko huo,Eugen Mikongoti, wakati akizungumza na umoja wa madereva taxi wilaya ya Ilala (Umatawi), jana jijini Dar es Salaam na kusema kuwa kwa sasa mfuko huo upo katika mchakato wa kufikisha huduma zake kwa karibu na vikundi vidogovidogo vikiwemo vya mama ntilie na vinginevyo.
”Tupo hapa kwa ajili ya kutoa elimu kwa madereva taxi wapatao 380 Wilaya ya Ilala kuhusiana na huduma za mfuko huu ili nao wawe mawakala kwa kuwashauri wenziwao kujiunga,”alisema Mikongoti.
Akizungumzia taratibu za kujiunga na vikundi hivyo,Mikongoti alisema kikundi kinapaswa kuwa na watu wapatao 12 au 15 lengo kuu likiwa ni kuwafikia kwa urahisi tofauti na mtu mmoja na kuongeza kuwa huwa wanashirikiana na taaisisi mbalimbali za kifedha zikiwamo benki pamoja na Vicoba katika kutoa huduma zao.
Naye Katibu Mtendaji wa umoja wa madereva taxi ilala, Khamisi Kivugo, alisema kuwa madereva taxi wengi jijini Dar es salaam hawajajiunga na mfuko huo wa Taifa wa bima ya afya hivyo ni fursa pekee kuweza kujitokeza na kujisajili.
Kutokana na hilo,Kivugo alisema madereva wengi pindi wanapopata ajali au kuumwa hukumbwa na wakati mgumu wanapokwenda hospitalini kwa ajili ya kupata tiba jambo ambalo wananchi wengi wamekuwa hawafurahishwi na kitendo hicho.
Aidha Kivugo alitoa rai kwa madereva wote kutopuuzia kujiunga na mfuko huo kwani ni mkombozi kwasabau hurahisisha huduma za matibabu na si jambo jema kwa yeyote kudharau kujiunga na mfuko huo kwa ajili ya ustawi wa fya.

No comments: