WENGI WAHAMASIKA KATIKA MATEMBEZI YA KUPIGA VITA MAUAJI YA ALBINO - IMETOSHA, JIJINI DAR


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe na Mbunge wa Viti Maalum, Al Shaymar Kweigyr wakiongoza matembezi ya hamasa ya kupiga vita mauaji ya albino nchini yaliyofanyika jana jijini Dar es salaam kuanzia viwanja vya Biafra mpaka Leaders Club, Kinondoni jijini Dar es salaam.
Matembezi yakiendelea.
Wadau kutoka sekta mbali mbali wakishiriki kwenye Matembezi ya hamasa ya kupiga vita mauaji ya albino nchini yaliyofanyika leo jijini Dar es salaam kuanzia viwanja vya Biafra mpaka Leaders Club, Kinondoni jijini Dar es salaam.Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe, Mbunge wa Viti Maalum, Al Shaymar Kweigyr, Balozi wa Harakati ya Imetosha, Henry Mdimu, Mwakilishi wa Chama cha Albino Tanzania (TAS), Abdillah Omar sambamaba na wadau wengine wakishiriki kuimba wimbo 'Tanzania Tanzania' kabla ya kuanza kwa shughuli nzima ya hamasa ya kupiga vita mauaji ya albino nchini, iliyofanyika jana kwenye viwanja vya Leaders Club, jijini Dar es salaam.
Mbunge wa Viti Maalum, Al Shaymar Kweigyr akicheza muziki wa sambamba na Mwanamuziki wa Reggae,Jhiko Manyika "Jhikoman" wakati wa shughuli nzima ya hamasa ya kupiga vita mauaji ya albino nchini, iliyofanyika leo kwenye viwanja vya Leaders Club, jijini Dar es salaam. Kulia ni Mwenyekiti wa Tanzania Bloggers Network ambao ni wadau wakubwa wa harakati ya Imetosha, Joachim Mushi.
Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Matembezi ya Hamasa ya kupiga vita mauaji ya albino nchini (Imetosha), Ally Masoud "Kipanya" akimkaribisha Balozi wa Harakati ya Imetosha, Henry Mdimu ili kuzungumza na Watanzania waliofika kwenye Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni jijini Dar es salaam jana.

Comments