RAis Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na mmiliki wa Azam TV ambayo ni kundi la makampuni ya SS Bkhresa, Said Salim Bakhresa, (watatu kushoto waliokaa), waziri wa habari, utamaduni, vijana na michezo, Dkt. Fenella Mukangara, (katikati aliyejifunga kitambaa), naibu mkurugenzi wa Azam TV, Tido Muhando, (wakwanza kushoto) na baadhi ya wafanyakazi wa TV hiyo mara baada ya Rais kuizindua rasmi Ijumaa Machi 6, 2015. TV hiyo yenye studio zake, barabara ya Mandela jijini Dar es Salaam, ni maarufu kwa vipindi vya michezo hususan soka
Rais Kikwete, akiwa ameketi na Mwen yekiti wa makampuni ya SS Bakhresa, Said Salim Bakhresa |
Rais akiwa kwenye mahojiano na Naibu Mkurugenzi wa TV hiyo, Tido Muhando |
Said Salim Bakhresa, (kushoto), akimpa maelezo Rais Kikwete.
|
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitangaza rasmi kuzinduliwa kwa studio mpya za stesheni ya Azam TV Tabata Relini jijini Dar es salaam Machi 6, 2015. Pamoja naye kwenye kilinge cha utangazaji ni mmiliki wa stesheni hiyo Bw. Saidi Salim Bakhressa.(PICHA NA IKULU)
RAis Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt Fenella Mukangara pamoja na uongozi na baadhi ya wafanyakazi wa Azam TV wakati wa sherehe za uzinduzi rasmi wa studio mpya za stesheni hiyo iliyopo Tabata Relini jijini Dar es salaam Machi 6, 2015.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo kutoka kwa fundi mitambo Mkuu wa Azam TV Bw. Mehdoub al Hadad juu ya namna gari la kurusha matangazo nje ya studio (OB Van) linavyofanya kazi wakati wa sherehe za uzinduzi rasmi wa studio mpya za stesheni hiyo iliyopo Tabata Relini jijini Dar es salaam Machi 6, 2015.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt Fenella Mukangara pamoja na uongozi na baadhi ya wafanyakazi wa Azam TV wakati wa sherehe za uzinduzi rasmi wa studio mpya za stesheni hiyo iliyopo Tabata Relini jijini Dar es salaam Machi 6, 2015.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt Fenella Mukangara wakitmbezwa sehemu mbali mbali za Azam TV na mwenyeji wao Bw. Saidi Salim Bakhressa wakati wa sherehe za uzinduzi rasmi wa studio mpya za stesheni hiyo iliyopo Tabata Relini jijini Dar es salaam Machi 6, 2015.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokewa na Bw. Saidi Salim Bakhressa wakati alipohudhuria sherehe za uzinduzi rasmi wa studio mpya za stesheni hiyo iliyopo Tabata Relini jijini Dar es salaam Machi 6, 2015.
PICHA NA IKULU
Comments