Mbunge wa jimbo la Kongwa mkoani Dodoma, Job Ndugai, (katikati), akizungumza kwenye mkutano wa hadhara aliouitisha jimboni kwake ambapo Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi CCM, Abdulrahman Kinana alikuwa mgeni rasmi kwenye mkutano huo, ambao Kinana licha ya kuuhutubia, alizindua miradi mbalimbali ikiwa ni pamoja na kushiriki shughul;i za kilimo na ujenzi. Ndugai ambaye pia ni Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, amekuwa akitajwa kwenye mitandao ya kijamii kuwa yu mgonjwa baada ya kuwa jkimya muda mrefu. Taarifa hizo mitandaoni zilipelekea Ofisi ya Bunge kutoa taarifa kuwa kiongozi huyo ni mgonjwa na wanaosema kuwa anaumwa ni wazushi wa kuipitiliza. Katika taarifa ya Ofisi ya Bunge, ilieleza kuwa Ndugai yuko bize jimboni kwake akijiandaa kumpokea bosi wake katika Chama Cha Ma[pinduzi yaani Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana. Katika kuonyesha nguvu alizonazo jimboni, umati mkubwa wa watu ulihudhuria kwenye mkutano aliouhutubia Kinana, na kumfanya apigwe na butwaa kwani katika ziara aliyoianza mapema wiki hii mkoani Dodoma, hajawahi kushuhudia umati kama huo.
Vigogo wa CCM, na wakulima watatu, wakiongozwa Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana(watatu kushoto aliyevua viatu), wakishiriki kilimo jimboni Kongwa |
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ufyatuaji wa matofali ya kujengea mabweni ya watoto wenye mahitaji maalum katika shule ya msingi Mlali B
|
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akifungua maji kwenye kituo cha Mlali wilaya ya Kongwa.
|
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, (wakwanza kushoto), na baadhi ya viongozi wa CCM, akienda sambamba wakati wa kulima shamba la mfano huko Kongwa |
Comments