Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kazi ya kuvuna Mpunga na Mbunge wa jimbo la Moshi Vijijini Dr. Cyril Chami na Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Mh. Leonidas Gama wakati katibu mkuu huyo alipotembelea mashamba ya umwagiliaji ya Mabogini Moshi Vijijini, ambapo amekagua miradi mbalimbali ya maendeleo na kushiriki katika kazi mbalimbali za mikono pamoja na wananchi, Kinana yuko katika ziara ya kikazi mkoani Kilimanjaro akikagua, kuhimiza na kusimamia utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM akiongozana na Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi. (PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-MOSHI VIJIJINI-KILIMANJARO)Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na viongozi wenzake wakiendelea na kazi ya kuvuna mpunga.Mpunga ukiwa umestawi katika mashamba hayo.Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiongozana na Mkuu wa wilaya ya Moshi mjini Ndugu Novatus Makunga kulia wakati walipowasili katika kata ya Mabogini.Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na wananchi mbalimbali wa kata ya Mabogini.Mbunge wa jimbo la Moshi Vijijini Mh. Dr. Cyril Chami akizungumza na wananchi wa kata ya Mabogini.Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akwahutubia wananchi katika kata ya Mabogini Moshi Vijijini wakati alipowatembelea.Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisaini kitabu cha wageni huku akizungumza na Mkuu wa Chuo cha Ufundi cha Kibosho Maadam Anna na kulia ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kilimanjaro Ndugu Iddi Juma.Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wanafunzi wa Chuo cha Ufundi cha Kibosho na walimu pamoja na wananchi wakati alipotembelea chuo hicho ambacho kimejengwa kwa nguvu za wananchi na marafiki wa Kibosho Education Trust Fund pamoja na Mbunge wa jimbo hilo Mh. Dr. Cyril Chami.Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipanda mti katika chuo cha ufundi cha Kibosho.Wasanii wakiimba wimbo kumkaribisha Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wakati alipowasili katika kata ya Kibosho Kati kwa ajili ya mkutano wa hadhara.Wasanii wakiimba wimbo kumkaribisha Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wakati alipowasili katika kata ya Kibosho Kati kwa ajili ya mkutano wa hadhara.
Comments