RAIS ROBERT MUGABE WA ZIMBABWE AWASILI ARUSHA TAYARI KWA KUFUNGUA MKUTANO WA VIJANA VIONGOZI WA CHINA NA AFRIKA NGURUDOTO
Rais wa Zimbabwe Mh. Robert Mugabe akishuka kwenye Ndege wakati alipowasili kwenye uwanja wa Ndege wa Kilimanjaro International Airport (KIA) tayari kwa kuufungua mkutano wa Vijana Viongozi wa Afrika na China (African- China Young Leaders Forum) unaofanyika kwenye hoteli ya Ngurudoto Mkoani Arusha kwa siku 4 ukijumuisha vijana kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika na China, Mzee Robert Mugabe amepokelewa na Makamu wa Rais Mh. Dr. Gharib Bilal na Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana na viongozi mbalimbali wa CCM na serikali mkoani Arusha.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-ARUSHA)Rais Robert Mugabe akipokea shada la maua mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa Ndege wa KIA leo tayari kwa kufungua mkutano wa Vijana Viongozi wa Afrika na China unaofanyika Ngurudoto mkoani Arusha kulia ni mwenyeji wake Makamu wa Rais Dr. Gharib Bilal aliyempokea.Rais wa Zimbabwe Mh. Robert Mugabe akisalimiana na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa Ndege wa KIA mkoani Arusha.Rais wa Zimbabwe Mh. Robert Mugabe akiongozana na mwenyeji wake Makamu wa Rais Dr. Gharib Bilal mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa KIA.Rais wa Zimbabwe Mh. Robert Mugabe akiongozana na Mwenyeji wake Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dr. Gharib Bilal.Rais wa Zimbabwe Mh. Robert Mugabe na Mwenyeji wake Makamu wa Rais Dr. Gharib Bilal wakiangalia vikundi vya ngoma vilivyokuwa vikitumbuiza wakati wa mapokezi, kushoto ni Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.Rais wa Zimbabwe Mh. Robert Mugabe akiteta jambo na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wakati walipokuwa wakiangalia vikundi vya ngoma vikitoa burudani.Rais wa Zimbabwe Mh. Robert Mugabe, Makamu wa Rais Dr. Gharib Bilal na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kushoto wakiangalia vikundi vya ngoma.Rais Mugabe na mwenyeji wake Mamaku wa Rais Dr. Gharib Bilal pamoja na viongozi wengine wakielekea kwenye chumba cha mapumziko kwenye uwanja wa Ndege wa KIA.Mwenyekiti wa Kamati ya Maandaliazi Mh. Steven Masele akizungumza na vyombo vyahabari kwenye uwanja wa KIA mara baada ya kuwasili kwa Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe.
Comments