Wednesday, March 04, 2015

RAIS KIKWETE AONGOZA MAZISHI YA KAPTENI DAMIANO KOMBA KIJIJINI LITUHI JANA


Askofu wa Kanisa Katoliki jimbo la Mbinga Mhashamu John Ndimbo akiongoza ibada ya mazishi ya aliyekuwa mbunge wa Mbinga Magharibi marehemu Kapteni John Damiano Komba wakati wa ibada ya mazishi yake yaliyofanyika kijijini kwake Lituhi wilayani Nyasa Mkoani Ruvuma jana.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakiweka udongo katika kaburi la aliyekuwa mbunge wa Mbinga Magharibi marehemu Kapteni John Damiano Komba wakati wa ibada ya mazishi yake yaliyofanyika kijijini kwake Lituhi wilayani Nyasa, Mkoani Ruvuma.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakiweka shada la maua katika kaburi la aliyekuwa mbunge wa Mbinga Magharibi marehemu Kapteni John Damiano Komba wakati wa ibada ya mazishi yake yaliyofanyika kijijini kwake Lituhi wilayani Nyasa, Mkoani Ruvuma.

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiongozana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye,Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana Ndugu Sixtus Mapunda  pamoja na wananchi kutoka maeneo mbali mbali ya Tanzania kwenda kumzika marehemu Kapteni John Komba kijijini kwake Lituhi.
Mke wa Marehemu Kapteni John Komba ,Salome (kushoto) akiweka shada la maua juu ya kaburi la marehemu.
Watoto wa marehemu Kapteni John Komba wakiweka shada la maua juu ya kaburi la Baba yao.
Watoto wa marehemu wakilia kwa uchungu wakati wa kuweka shada la maua kwenye kaburi la Baba yao .

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiweka shada la maua kwenye kaburi la Kapteni John Damian Komba aliyezikwa kijijini kwake Lituhi.
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara) Mwigulu Lameck Mchemba pamoja na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa Nape Nnauye wakiweka shada la maua juu ya kaburi la Kapteni John Komba aliyefariki jijini Dar es Salaam tarehe 28 februari na kuzikwa kijijini kwake Lituhi tarehe 3 Machi 2015.
Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Ndugu Said Mwambungu (kulia) akiweka shada la maua pamoja na mkewe kwenye kaburi la Kapteni John Komba.
Khadija Kopa akiwa katika huzuni kubwa mara baada ya kuweka shada la maua kwenye kaburi la Kapteni John Komba kijijini kwake Lituhi.
(Picha: Freddy Maro)

No comments: