Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa barabara ya Mwanama- Olorien ambayo itajengwa kwa kiwango cha lami, Ndugu Kinana pia aliitembelea na kuikagua barabara hiyo.
Ujenzi wa barabara ya Mwanama- Olorien ambayo itajengwa kwa kiwango cha lami ukindelea ambapo Ndugu Kinana pia aliitembelea na kuikagua.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akitembelea kiwanda cha General Tyre eneo la Themi,jijini Arusha,ambapo Kiwanda hicho Serikali imeamua kukifufua na kuanza kuzalisha upya bidhaa zake kupitia shirika la Maendeleo la Taifa (NDC),pichani kati ni Kaimu Mkuregunzi wa NDC,Bwa.Mlingi Mkucha na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Arusha,Onesmo Ole Nangolo.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akisikiliza malalamiko ya baadhi ya waliokuwa wafanyakazi wa kiwanda cha shirika la General Tyre,ambao Ndugu Kinana ameahidi kuyafanyia kazi na kuhakikisha wafanyakazi hao wanapata haki yao.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa ameambatana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye sambamba na viongozi wengine wa chama hicho wakitembelea kiwanda cha nguo cha Kiltex,ambapo kimefungwa na kusimamisha uendeshaji wake,ambapo kwa miaka mitatu kiwanda hicho kiligeuzwa kuwa ghala la kuhifadhia nafaka,hku mitambo yake yote ikiwa imeondolewa na kupelekwa kusikojulikana,
Mlinzi Mkuu wa Kiwanda cha Kiltex,Mathias Mahundi akifafanua jambo kwa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana,na kulia ni Mkuu mpya wa Wilaya ya Arumeru na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mh.Asnah Mwilima.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akizunguza na Halmashauri kuu ya CCM Wilaya,mapema leo jijin Arusha,ambapo pia alipokea taarifa za kazi ya chama na serikali.
Comments