Tuesday, March 24, 2015

MKUU WA WILAYA YA KALAMBO AMUWAKIILISHA MKUU WA MKOA WA RUKWA KATIKA KILELE CHA WIKI YA MAJI MKOANI RUKWA KATIKA KIJIJI CHA KINAMBO NA KUZINDUA MRADI WA MAJI

Mkuu wa Wilaya ya Kalambo Mhe. Willman Kapenjama akikagua chanzo cha Maji katika Kijiji cha Kinambo Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Maji Mkoani Rukwa tarehe 22/03/2015 . Mkuu huyo wa Wilaya alimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya ambaye yupo nje ya Mkoa huo kikazi. Chanzo hicho cha Maji kinatumiwa na vijiji vitatu vya Kinambo, Lianza na Maenje ambapo jumla ya vituo 23 vya kuchotea maji vimejengwa katika vijiji hivyo ambavyo vitahudumia zaidi ya kaya 5,304. Mradi huo ambao ni sehemu ya miradi ya maendeleo ya Matokeo Makubwa Sasa (BRN) umekamilika ndani ya wakati (Miezi 6 ya Mradi) na umegharimu zaidi ya fedha za kitanzania Milioni 300. Kaulimbiu ya maadhimisho hayo ni “Tekeleza sasa kwa Matokeo makubwa”
Washiriki mbalimbali wa Kilele hicho cha Wiki ya Maji walifika kujionea chanzo hicho cha maji ambacho ni cha asili na hakitumii pampu kusukuma maji kutokana na kuwepo eneo la milimani.
 Mhe. Kapenjama akizindua mradi huo wa Maji.
Mradi huo wa Maji ni pamoja na tanki la kuhifadhia Maji lenye ujazo wa lita laki moja.
 Mkuu wa Wilaya ya Kalambo Mhe. Willman Kapenjama akihakikisha uwepo wa maji katika moja ya vituo vya kuchotea maji katika kijiji cha Kanambo.
Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Bi. Emmy George akimkaribisha Mkuu wa Wilaya ya Kalambo Mhe. Willman Kapenjama kuzungumza na wananchi wa Vijiji vya Kinambo, Lianza na Maenje. Mkuu huyo wa Wilaya aliwataka wananchi wa vijiji hivyo kuithamini Serikali iliyopo madarakani kwa mchango mkubwa wa kupeleka huduma mbalimbali kwa wananchi wake, hata hivyo aliwaomba kuwa mstari wa mbele katika kutunza mradi huo pamoja na kuhifadhi vyanzo vya maji.
 Kikundi cha Ngoma za asili cha Wasukuma kikitumbuiza katika Maadhimisho hayo.
Mcheza ngoma akitumbuiza kwa staili ya aina yake akiwa ameshikilia pipa kwa mdomo huku akicheza ngoma ya asili ya kikundi cha Kinambo. 
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Rukwa Mhe. Hyporatus Matete akitoa salam za chama katika maadhimisho hayo. Alisema kuwa kazi ya Chama hicho ni kuisimamia Serikali iliyopo madarakani jambo ambalo limekuwa na matunda makubwa katika utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya CCM ambayo kwa kiasi kikubwa imetekelezwa na inaendelea kutekelezwa ambapo ni pamoja na miradi mbalimbali yenye kutoa huduma kwa wananchi.
 Katibu Mwenezi wa CCM Mkoa wa Rukwa Ndugu Clemence Bakuli akitoa salam za Chama katika Maadhimisho hayo.
 Ndugu Shaban Suleiman Mhandisi wa Maji Sekretarieti ya Mkoa wa Rukwa akisoma risala ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya Maji Mkoani humo.
(Na Hamza Temba – Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa@Rukwareview.blogspot.com)

No comments: