Saturday, March 28, 2015

Waziri wa Ardhi, Nyumba na MAendeleo ya Makazi William Lukuvi ashughulikia migogoro ya Ardhi Morogoro

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Vangimembe Lukuvi akizungumzia migogoro ya ardhi ya mkoa wa Morogoro ambapo kwa siku nzima ya leo alipata fursa ya kusikiliza taarifa ya migogoro ya ardhi ya mkoa huo na kisha kupata fursa ya kukusanya karatasi za kero za migogoro ya ardhi kisha kuzikabidhi kwa timu ya wataalamu ambao watazichambua na kutoa mapendekezo kwa waziri jinsi ya kuzitatua pia ameagiza ofisi za Msajili wa Ardhi Kanda ya Mashariki kujengwa na kuhamishiwa Mororgoro.
Mbunge wa Viti Maalumu Susan Kiwanga akizungumzia masuala ya migogoro yanayoukabili mkoa wa Morogoro sambamba na njia ambazo zitasaidia kuondokana na migogoro hiyo 
 Mstahiki Meya wa Manispaa ya Morogoro, Amiri Nondo akifuatilia mjadala huo kulia kushoto kwake ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Morogoro, Innocent Kalogeris.
 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Vangimembe Lukuvi akizungumzia migogoro ya ardhi ya mkoa wa Morogoro
 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Vangimembe Lukuvi akizungumzia migogoro ya ardhi ya mkoa wa Morogoro
 Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro, Leonard Paulo, akizungumzia changamoto zinazowakabili katika kukabiliana na migogoro ya ardhi mkoani Morogoro.
 Mbunge wa Jimbo la Morogoro Kusini Mashariki, Lucy Nkya akizungumzia kero zinazowakabili katika eneo lao.
>
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Morogoro, Innocent Kalogeris akizungumzia hali ya migogoro ya ardhi kwa mkoa wa Morogoro wakati Waziri Lukuvi alipokuwa akisikiliza kero mbalimbali za ardhi kwa wananchi wa mkoa wa Morogoro.

 Mbunge wa Ulanga Magharibi, Dk. Haji Mponda akizungumzia kero zinazowakabili katika eneo lao
a wa Morogoro.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro, Theresia Mahongo akikagua karatasi zenye kero za migogoro ya ardhi zilizokuwa zikikabidhiwa kwake kwaajili ya kukabidhi kwa Waziri Lukuvi.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Vangimembe Lukuvi akipokea makaratasi yaliyoandikwa malalamiko ya wananchi wa mkoa wa Morogoro leo mchana katika ziara yake aliyofanya mkoani humo.
 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Vangimembe Lukuvi akipokea makaratasi ya malalamiko ya wananchi wa mkoa wa Morogoro leo mchana katika ziara yake aliyofanya mkoani humo kushoto kwake ni  Mbunge wa Morogoro Mjini Aziz Aboud.

No comments: