Meneja wa kiwanda cha Bia cha TBL Mbeya, Waziri Jemedari akizungumza na waandishi wa habari wa Mkoa wa Mbeya(hawapo pichani) walipofanya ziara na kushiriki shindano la kuonja bia hivi karibuni.
Meneja mawasiliano na Uhusiano wa TBL, Editha Mushi akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari Mbeya. |
Meneja mauzo na usambazaji nyanda za juu kusini VIvianus Rwezaura, akimkabidhi zawadi Keneth Ngelesi ambaye aliibuka mshindi wa pili kwa kujikusanyia alama nne kwa tano.
|
Washindi wakiwa na zawadi zao.
|
Mwakilishi wa gazeti la Tanzania daima Mbeya, Christopher Nyenyembe akijaza fomu ya mashindano.
|
.Mtangazaji wa redio ya Mbeya fm Fredy Jackson (kushoto) akiuliza maswali kutoka kwa Saada Matiku ambaye alikuwa mshindi wa kwanza lakini bado alipata sifuri. |
Mwandishi wa habari wa gazeti la Habari Leo, Joackim Nyambo akiwa sambamba na Mmiliki wa mtandao wa Mbeya yetu, Joseph Mwaisango wakifuatilia kwa makini katika mashindano ya kuonja bia.
|
Waandhishi wa Habari wa Mkoa wa Mbeya wakiwa kwenye chumba cha mashindano ya kuonja bia.
|
Meneja rasilimali watu George Albano akitoa somo kwa waandishi wa habari mkoa wa Mbeya |
Waandhishi wa habari Mbeya wakipata maelezo mbali mbali kuhusiana na kiwanda cha bia cha TBL.
|
.Waandishi wa habari Mbeya wakielekea kutembelea mitambo ya kuzalisha bia kiwandani hapo.
|
.Meneja wa Kiwanda akitoa maelekezo.
|
Waandishi wa Habari wakipata maelekezo mbali mbali juu ya uzalishaji wa bia.
|
Baadhi ya Wataalamu wa Kiwanda cha Bia cha TBL wakiendelea na majukumu yao. |
Muonekano wa Kiwanda |
Picha ya pamoja baada ya kumaliza Ziara. |
……………………………………………………………………………………………
WAANDISHI wa Habari Mkoa wa Mbeya hivi karibuni walifanya ziara ya kutembelea kiwanda cha bia TBL Mbeya ambapo pia walipata nafasi ya kushiriki mashindano ya kuonja bia.
Katika shindano hilo, Mzoefu Saada Matiku ambaye ni mwandishi wa Chanel Ten aliibuka kidedea kwa kupata alama tano kwa tano ikiwa ni mara ya pili tangu apate nafasi kama hiyo kwenye mashindano ya mwaka juzi.
washindi wengine ni Kenneth Ngelesi wa Tanzania Daima aliyeibuka mshindi wa pili huku Merali Chawe wa Daily news akiibuka kidedea katika nafasi ya tatu.
Mbali na mashindano hayo Uongozi wa Kiwanda hicho umeilalamikia Serikali kwa kitendo cha kupandisha ushuru kwenye vinywaji katika kila mwaka wa bajeti jambo linaloathiri uzalishaji kwa makampuni binafsi.
Hayo yalibainishwa na Meneja wa Kampuni ya Bia Tanzania(TBL) Kiwanda cha Mbeya, Waziri Jemedari, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari walipofanya ziara kiwandani hapo Iyunga jijini Mbeya.
Jemedari alisema uzalishaji wa bidhaa zao katika kiwanda cha Mbeya umepungua kutokana na ongezeko la Kodi ambapo awali kabla ya kupandishiwa kwa kodi hiyo Kiwanda kilikuwa kinafanya kazi masaa 24 kwa siku 7 lakini sasa kinafanya kazi masaa 24 kwa siku tatu.
Alisema hadi sasa uzalishaji huo umepungua kwa asilimia 40 ambapo wakati mwingine hulazimika kuzima na kupumzisha mitambo sababu kubwa ni kupungua kwa mauzo baada ya bei kuongezeka.
Alisema uzalishaji ulikuwa ni Hektolita 12000 hadi 6000 kwa siku lakini sasa hivi umeshuka hadi Hektolita 400 hivyo kusababisha hata kutishia kupunguza watumishi.
Alisema kitendo cha serikali kupandisha bei kwa mlaji kinaathiri pande nyingi ambapo Mlaji mwenyewe nashindwa kumudu gharama za kununua bidhaa ili hali mzalishaji anaweza anakazalisha kwa wingi lakini sokoni zisinunuliwe.
“Kama mnavyoona hizo zote ni chupa tupu ambazo zimekosa vinywaji na zilipaswa kuwepo sokoni na hii ni kutokana na kupandisha kodi kiholela, jambo ambalo hata Serikali haijatambua kuwa na yenyewe imekosa mapato” alisema Meneja huyo huku akionesha chupa tupu za bia.
Aliongeza kuwa serikali ilipaswa kumpandishia kodi mzalishaji na sio mlaji wa mwisho jambo ambalo linaathiri uchumi wa mtu mmoja mmoja.
Alisema kwa kufanya hivyo ingekuwa rahisi kwa mzalishaji kuwa na mbinu mbadala ya kukusanya kodi kwa ajili ya kuilipa Serikali tofauti na ilivyosasa ambapo Serikali huongeza gharama ya kodi kwenye bidhaa inayopaswa kwenda sokoni.
Jemedari alisema katika kunusuru kiwanda kisifungwe uongozi wa tbl umelazimika kupunguza bei ya vinywaji tofauti na bei elekezi inayotakiwa kutokana na kiwango cha kodi ya serikali ambapo Bia moja ilipaswa kuuzwa 2500 lakini kiwanda kimepunguza hadi shilingi 2200.
Na Mbeya yetu
Comments