(Picha na: Genofeva Matemu – Maelezo)
……………………………………………………………..
Na: Genofeva Matemu – Maelezo
Maafisa Utamaduni na wadau wa utamaduni wametakiwa kuuenzi utamaduni wa watanzania kwa kutekeleza na kusimamia utamaduni ulio sahihi na kuacha kuiga tamaduni zisizokuwa zetu.
Rai hiyo imetolewa jana jijini Dar es Salaam na mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala Bw. Raymond Mushi alipokua akifunga kikao kazi cha kumi cha Maafisa Utamaduni kutoka Halmashauri zote Tanzania Bara.
Bw. Mushi amesema kuwa kikao kazi hicho kilichosimamia kauli mbiu isemayo Fani za Sanaa zielimishe Umma Maudhui ya Katiba pendekezwa kimefanyika wakati muafaka hasa ukizingatia taifa lipo kwenye hatua ya kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura ambalo litatumika pia kupigia kura katiba pendekezwa.
“Sanaa ni shughuli pana kwa kuwa inaweza kufikisha ujumbe kwa haraka katika jamii hasa kwa kutumia fani mbalimbali kama muziki, ngojera, ngoma, maigizo na kadhalika hivyo kwa kupitia fani za Sanaa Umma utaelewa maudhui ya katiba pendekezwa na kufanya maamuzi sahihi ya kuipigia kura katiba pendekezwa”, alisema Bw. Mushi.
Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Idara ya Utamaduni Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Afisa Utamaduni Bw. Habibu Msami amesema kuwa kikao kazi cha kumi cha Sekta ya Utamaduni kimekuwa na mafanikio chanya kwani washiriki wamepata fursa ya kujadili kwa kina masuala mtambuko yanayoikabili sekta hiyo.
“Ni hakika kuwa tutakapotoka hapa tutakua mfano mzuri katika Halmashauri na Asasi zetu kwa kuzingatia mambo ya msingi na kuhakikisha tunautetea, tunaulinda na kuuendeleza utamaduni wetu kwa ajili ya ujenzi wa Taifa”, alisema Bw. Msami.
Naye Afisa Utamaduni kutoka Kiteto Bibi. Bihawa Masawika amesema kuwa kikao kazi cha sekta ya utamaduni kimewawezesha kupata maarifa yatakayowawezesha kuwa wahamasishaji wakubwa na kuwa chachu na mabalozi wazuri katika kutekeleza na kuendeleza masuala ya utamaduni nchini.

No comments:
Post a Comment