MATUKIO BUNGENI MJINI DODOMA

1
Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera,Uratibu na Bunge)Mhe.Jenista Mhagama akisoma Muswada wa Sheria ya Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania kwa mara ya pili katika Bunge,Mjini Dodoma
2
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe.Asha Migiro (kushoto)akimsikiliza kwa makini Naibu Waziri wa Fedha Mhe.Mwigulu Nchemba ndani ya Ukumbi wa Bunge wakati wa kikao cha nane cha bunge .
3
Mhe.Lediana Mng’ong’o Viti Maalum CCM akitoa maoni yake katika kipindi cha uchangia wa mada kuhusu Muswada wa Sheria ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania,ndani ya Bunge Mjini Dodoma.
4
Mhe.Edward Lowassa (Mb) wa Monduli (kushoto)akizungumza na Mhe.Muhammed Seif Khatib (Mb) wa Uzini ndani ya ukumbi wa bunge jijini Dodoma wakati wa kikao cha Bunge
5
Waziri wa Maji Mhe.Prof.Jumanne Maghembe (wakwanza kushoto) akisalimiana na Naibu Waziri Waziri wa Fedha Mhe.Adam Malima nje ya Ukumbi wa Bunge jijini Dodoma,katikati ni Mhe.Lucy Nkya Mb Morogoro Vijijini.
6
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Anne Makinda akizungumza nje ya Ukumbi wa Bunge Mjini Dodoma na Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera,Uratibu na Bunge) Mhe.Jenista Mhagama.

Comments