DAKTARI WA SHIRIKA LA WAMISIONARI AWAPIMA AFYA VIJANA WAATHIRIKA WA MADAWA YA KULEVYA

01
Daktari wa Shirika la Wamisionari  (Medical Missionaries lifestyle center for East Afrika) Kefa  Omari akimpima afya ya mwili mzima kijana Francis Oni ambaye ni Mwathirika wa madawa ya kulevya anaeishi katika kituo cha Gola Foundation kilichopo kijiji cha Njoro wilaya ya Arumeru kinachojishughulisha na watoto na vijana ambao ni  waathirika wa madawa hayo,kipimo cha kisasa kinachotumia kompyuta kitaalamu kinaitwa (QMA). Daktari huyo alifika katika kituo hicho jana na  kutoa msaada wa kitabibu kwa vijana hao pamoja na madawa ya kuondoa sumu inayotokana na madawa hayo katika mwili.Picha na Mahmoud Ahmad Arusha
02
Daktari wa Shirika la Wamisionari  (Medical Missionaries lifestyle center for East Afrika) Kefa  Omari akitoa elimu kwa vijana ambao ni waathirika
wa madawa 
wanaoishi katika kituo cha Gola Foundation kilichopo kijiji cha Njoro wilaya ya Arumeru kinachojishughulisha na watoto na vijana ambao ni  waathirika wa madawa hayo, Daktari huyo alifika katika kituo hicho jana na  kutoa msaada wa kitabibu kwa vijana hao pamoja na madawa ya kuondoa sumu inayotokana na madawa hayo katika mwili,katikati ni  Mkurugenzi wa Shirika hilo Elisha Maghembe Picha na Mahmoud Ahmad Arusha
……………………………………………………..
Taasisi isiyo ya kiserikali inayojihusisha na watoto  wanaoishi katika mazingira magumu jijini Arusha Gola Foundation imeanzisha kitengo cha kuwasaidia watoto na vijana ambao ni waathirika wa madawa ya kulevya ili wapate matibabu na kuachana na matumizi ya dawa hizo na kuweza kushiriki vyema katika shughuli za kiuchumi na kijamii.
 
Mkurugenzi wa Shirika hilo Elisha Maghembe amesema kuwa kwasasa wanacho kituo cha watoto na vijana 25 wa mitaani ambao wameanza kupatiwa matibabu kituo ambacho kipo mbali na mji ili kuwatenga watoto hao na mazingira hatarishi ambayo huwashishi kurudi katika hali zao za awali.
 
Maghembe alisema kuwa katika kituo hicho vijana hao wanajishughulisha na shughuli za kilimo shughuli ambayo inawaingizia kipato hivyo kuwaepusha na vitendo vya uporaji  na biashara haramu.
 
Hivyo ameiomba jamii kuungana pamoja kuwasaidia watoto wa mitaani  ,wanaoishi kwenye mazingira magumu pamoja na waathirika wa madawa ya kulevya  na kuokoa vijana wenye nguvu,vipaji na uwezo mkubwa unaoteketea kwa madawa badala ya kuwa rasilimali ya taifa.
 
Daktari wa Shirika la Wamisionari  (Medical Missionaries lifestyle center for East Afrika) Kefa  Omari ambaye alifika katika kituo hicho jana na  kutoa msaada wa kitabibu kwa vijana hao pamoja na madawa ya kuondoa sumu inayotokana na madawa hayo katika mwili.
 
Kefa  ameshauri  vijana hao kuzingatia kanuni bora za afya ikiwemo kupata lishe bora,kuzingatia mazoezi,unywaji maji,kutenga muda kupumzika  kwasababu inawezekana kuachana kabisa na matumizi ya madawa hao na kurudi katika hali ya kawaida.
Kenedy Njenga na Francis Oni ni Vijana wanaoishi katika kituo hicho kilichopo Arumeru  wamesema kuwa kwasasa wameamua kuachana na madawa ya kulevya kwa kipindi kirefu wamekua wakiathirika kiafya na kiuchumi hivyo  wanatumia nafasi hiyo kufanya shughuli za kijamii kama kilimo pamoja na kujitolea .

Comments