Kinana amewaasa wana CCM kukemea vitendo vibaya vya viongozi wa serikali na watendaji wanaokiuka utaratibu wa kazi na kufanya mambo yasiyokuwa ya kimaadili katika utendaji wao. Ili kukiweka chama hicho katika sura nzuri kwa wananchi, “Wana CCM tunatakiwa kuwa wa kwanza kukemea maovu siyo wana CCM tunaanza kuwalinda na kuwatetea waovu jambo ambalo si sawa kabisa, Tutahakikisha tunairudisha CCM ya wanyonge na masikini watoto wa wakulima na wafanyakazi aliyoiacha Baba wa Taifa Mwalimu J.K.Nyerere”, Katika ziara hiyo Kinana anaongozana na Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-HAI-KILIMANJARO)



























No comments:
Post a Comment