Mkuu wa mkoa wa Manyara ,Mhe.Joel Nkaya Bendera akizungumza katika kikao cha viongozi wa wilaya zote za mkoa huo kilichofanyika ofisi ya Mkuu wa Mkoa mjini Babati,kushoto ni Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi,Mhe.William Lukuvi na kulia ni Mkuu wa wilaya ya Babati,Crispin Meela.Mhe.Bendera amesisitiza nidhamu ya kazi katika kuhudumia wananchi na ameapa kuwaondoa watendaji wabovu mkoani humo.
Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi,Mhe.William Lukuvi akizungumza katika kikao cha viongozi wa wilaya zote za mkoa wa Manyara kilichofanyika ofisi ya Mkuu wa Mkoa mjini Babati.Ameuagiza uongozi wa mkoa huo kumaliza migogoro ya ardhi ifikapo mwezi Mei mwaka huu.
Mratibu wa Tume ya Waziri Mkuu ya kuhakiki na kuweka mipaka kwenye maeneo yenye migogoro ya ardhi mkoani Manyara,ambaye pia ni Mrasimu Ramani Mwandamizi,Bw.Benedict Mugambi akitoa maelezo ya hatua waliyofikia katika kuweka mipaka mkoani Manyara na kusema kuwa migogoro mingi ya mipaka inasababishwa na wanasiasa.Baadhi ya watendaji wa sekta ya Ardhi Kanda ya Kaskazini na baadhi ya waheshimiwa wabunge akiwemo Mbunge wa Kiteto,Benedct Ole Nangoro na Mbunge wa Viti Maalum,Pauline Gekul wakifatilia maelekezo ya Mhe Lukuvi alipozungumza na watendaji wa mkoa wa Manyara jana.
Wananchi wa mkoa wa Manyara wakimsikiliza Waziri wa Ardhi(hayupo pichani)alipokutana nao kusikiliza kero za migogoro ya ardhi inayosababishwa na watendaji wa sekta hiyo kwenye ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Babati.
Wananchi wa mkoa wa Manyara wakipeana maelekezo yaliyotolewa na Waziri wa Ardhi ya namna ya kuwasilisha malalamiko yao kwa maandishi alipokutana nao kusikiliza kero za migogoro ya ardhi inayosababishwa na watendaji wa sekta hiyo kwenye ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Babati.
Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi,Mhe.William Lukuvi akizungumza na wananchi wa mji wa Babati waliojitokeza kuwasilisha kero zao zinahusu migogoro ya ardhi.Kikao hicho kilihudhuriwa pia na wabunge wa mkoa wa Manyara.
Baadhi ya watendaji wa wizara ya ardhi wakiratibu malalamiko ya wananchi katika kikao kilichofanyika ofisi za halmashauri ya wilaya ya Babati,mkoa wa Manyara.Katibu Tawala wa mkoa wa Manyara,Mhandisi Omar Chambo akisoma taarifa ya migogoro ya ardhi mkoani humo kwa Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi,Mhe.William Vangimembe Lukuvi kwenye ziara yake ya kusikiliza kero za ardhi.
Comments