Mama Mkimbizi kutoka nchini Kongo akiwa na mwanae, pamoja na wakimbizi wengine wakisubiria kwenda kufanyiwa uhakiki wa taarifa zao jana ili waweze kutambulika rasmi kuwa ni wakimbizi katika Kambi ya Nyarugusu, iliyopo Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma. Zaidi ya familia ya Wakimbizi 14,000 sawa na jumla ya Wakimbizi 68,000 wamefanyiwa uhakiki huo kambini hapo. Picha zote na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Mkuu wa Kambi ya Wakimbizi Nyarugusu, Sospeter Boyo (wapili kushoto) akiwahoji mafundi ujenzi ambao ni wakimbizi kutoka nchini Kongo, wakati wakilijenga darasa la Shule ya Sekondari Fraternite iliyopo katika Kambi ya Nyarugusu, wilayani Kasulu, Mkoa wa Kigoma. Shule hiyo inafundisha kwa kutumia Mitahala ya Elimu ya nchini Kongo. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Mratibu wa Idara ya Wakimbizi Kanda ya Kigoma, Tony Laiser (kulia) akimkabidhi Mkimbizi kutoka nchini Kongo katika Kambi ya Nyarugusu msaada wa taa inayotumia mionzi ya jua. Taa hiyo pia ina sehemu ya kuchajia simu za mikononi. Maelfu ya wakimbizi katika Kambi hiyo walipewa msaada huo jana ulitolewa na Shirika la Kimataifa la Kuhudumia Wakimbizi Duniani (UNHCR) kupitia Shirika linalotoa huduma za Kijami na Unyanyasaji wa Kijinsia (IRC) ikiwa ni kawaida yao kutoa misaada mbalimbali ya kuwasaidia wakimbizi hao waliopo katika kambi hiyo, Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Mratibu wa Idara ya Wakimbizi Kanda ya Kigoma, Tony Laiser (kulia) akimuhoji Mkimbizi kutoka nchini Burundi, Bibi Karumere (katikati) wakati wa kufanyiwa uhakiki wa taarifa zake ili aweze kutambulika rasmi kuwa ni Mkimbizi katika Kambi ya Nyarugusu, iliyopo Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma. Zaidi ya familia ya Wakimbizi 14,000 sawa na jumla ya Wakimbizi 68,000 wamefanyiwa uhakiki huo kambini hapo. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Mratibu wa Idara ya Wakimbizi Kanda ya Kigoma, Tony Laiser akiwaongoza Wakimbizi wazee kutoka nchini Kongo jana kufanyiwa uhakiki wa taarifa zao ili watambulike rasmi kuwa ni wakimbizi katika Kambi ya Nyarugusu, iliyopo Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma. Zaidi ya familia za Wakimbizi 14,000 ikiwa ni sawa na Wakimbizi 68,000 wamefanyiwa uhakiki huo kambini hapo. Picha zote na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Comments