TIMU YA MAJAJI KWA AJILI YA KUMTAFUTA MSHINDI WA TUZO YA RAIS YA HUDUMA ZA JAMII NA UWEZESHAJI YAANZA KAZI RASMI WILAYANI HANDENI MKOANI TANGA
Jaji
Venance Bahati ( kulia) na Jaji Constancia Gabusa (kushoto) wakijadiliana jinsi
ya kuanza zoezi la kumtafuta mshindi wa
Tuzo ya Rais ya Huduma za Jamii na Uwezeshaji nje ya
Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Handeni mara baada ya timu hiyo kuwasili katika wilaya ya Handeni
kwa ajili ya zoezi hilo. Zoezi hili
linahusisha makampuni yanayojishughulisha na shughuli za madini, gesi na mafuta
ambapo mshindi katika utoaji wa huduma
bora kwa jamii na uwezeshaji
atakabidhiwa tuzo yake mapema Novemba, mwaka huu.
Afisa
Mipango wa Halmashauri ya Handeni
Bw. Dawson Temu akielezea jinsi
makampuni ya utafutaji madini
yanavyochangia katika huduma za jamii katika wilaya ya Handeni mbele ya
timu ya majaji (hawapo pichani) ofisini kwake.
Jaji
Constancia Gabusa (kushoto) na Kaimu
Afisa Madini Mkazi wa Handeni Bw. Jared
Obado (kulia) wakifuatilia kwa makini maelezo yaliyokuwa yanatolewa na Afisa
Utawala wa Wilaya ya Handeni Upendo Magashi (hayupo pichani)
Jaji
Venance Bahati (kushoto) akikagua moja ya
ofisi za waalimu katika shule ya msingi ya Nyasa zilizojengwa na kampuni
ya utafutaji wa madini ya Canaco katika
zoezi la kutathmini miradi
iliyofadhiliwa na kampuni hiyo
Mmoja
wa wakazi wa kijiji cha Nyasa ( wa pili kutoka kulia) ambaye jina lake halikupatikana mara moja akielezea
mchango wa makampuni ya utafutaji wa
madini katika huduma za jamii ndani ya
kijiji hicho.
Mkuu
wa Mradi wa Kampuni ya Utafutaji wa
Madini ya Canaco Bw. John Holana (kulia) akielezea mchango wa
kampuni hiyo katika uendelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika kijiji
cha Nyasa ikiwa ni pamoja na maji, shule na mkakati wa kujenga kituo cha afya.
Kushoto ni mmoja wa majaji Bi. Constancia Gabusa.
Mkuu
wa Mradi wa Kampuni ya Utafutaji wa Madini ya Canaco Bw.
John Holana akitoa maelezo mbele ya majaji pamoja na wajumbe wengine wa
kijiji cha Nyasa mafanikio yaliyopatikana tangu kuanzishwa kwa kampuni hiyo.
Mjiolojia
Mkuu kutoka Kampuni ya Utafutaji wa Madini ya Douglas Lake Minerals
Bw. Godfrey Bitesigirwe akielezea
changamoto wanazokumbana nazo katika
utoaji wa huduma bora kwa jamii inayoizunguka kampuni hiyo mbele ya
majaji waliotembelea kampuni hiyo (hawapo pichani) kwa ajili ya kuendelea na
zoezi la kumtafuta mshindi wa Tuzo ya
Rais ya Huduma za Jamii na Uwezeshaji.
Jaji
Constancia Gabusa akitoa ushauri kwa
kampuni ya Utafutaji wa Madini ya Douglas
Lake Minerals jinsi ya kukabiliana na
changamoto katika utoaji wa huduma bora
kwa jamii inayowazunguka ikiwa ni pamoja na umuhimu wa kuwashirikisha wananchi
katika mipango ya miradi ya maendeleo
Mwalimu
Mkuu Msaidizi wa Shule ya Msingi ya Nyasa Bw.
Ali Mhada akielezea mchango wa
kampuni ya utafutaji wa madini ya Canaco katika kutoa ufadhili kwa wanafunzi
waliofanya vizuri kama mkakati mmojawapo
wa kuwajengea wanafunzi uwezo wa kuwa wataalamu wa baadaye na kufanya kazi
katika kampuni hiyo.
Comments