Basi la Sabena la Mbeya kwenda Mwanza na AM Dreamline ya Mwanza-Mpanda. Ajali hiyo imetokea maeneo ya Mlogolo takribani kilometa 4 to wilaya ya Sikonge.
Mashuhuda wanadai takribani watu kumi au zaidi wamepoteza maisha wakiwemo madereva. Maelezo baadhi ya mashuhuda wanadai dereva mmoja ameonekana kiwiliwili pekee na juhudi za kukisaka kichwa cha marehemu zinaendelea. Wameongeza zaidi kuwa yawezekana hata madereva hao walikuwa ni Day-worker (Daiwaka) kama ilivyozoeleka.
Wakati mtandao huu ukipokea taarifa ni kuwa hali si nzuri eneo la tukio na uokoaji wa majeruhi zaidi ya 30 unaendelea na kuwapeleka katika hospitali ya Mission ya wilayani Sikonge.
Inakadiriwa kuwa karibu robo tatu ya basi la sabena imeharibiwa vibaya sana.
Inakadiriwa kuwa karibu robo tatu ya basi la sabena imeharibiwa vibaya sana.
Mashuhuda wa ajali iliyohusisha mabasi mawili ya abiria kati ya Sabena ya Mbeya-Tabora na AM Dreamline ya Mwanza-Mpanda.
Baadhi ya miili ya marehemu.
Comments