MAMLAKA YA VIWANJA VYA NDEGE TANZANIA TAA YAKABIDHI MADAWATI 100 SHULE YA MSINGI YOMBO

 3a
Mkurugenzi wa Mamlaka ya viwanja vya Ndege Tanzania TAA Bw. Suleiman Suleiman akisaliiana na wanafunzi wa shule ya msingi Yombo mara baada ya kuwakabidhi madawati 100 yaliyotolewa na Mamlaka hiyo kwa ili kusaidia kuondoa upungufu wa madawati shuleni hapo.
6a
Mkurugenzi wa Mamlaka ya viwanja vya Ndege Tanzania TAA Bw. Suleiman Suleiman akimkabidhi Abdallah Ali Mmoja wa wanafunzi hao ambaye ni kiranja huku Mwalimu Mkuu Bi. Christina Kasyupa akishuhudia wa pili kutoka kushoto ni Celina Dismas Dada wa shule.
7a
Mkurugenzi wa Mamlaka ya viwanja vya Ndege Tanzania TAA Bw. Suleiman Suleiman ,Abdallah Ali Mmoja wa wanafunzi hao ambaye ni kiranja na Celina Dismas Dada wa shule wakiwa wamekaa kwenye dawati mara baada ya makabidhiano huku uongozi wa shule hiyo ukishuhudia tukio hilo.
a1
Kwaya ya shule hiyo ikitoa burudani
a4
Wanafuzi wakicheza ngoma.
…………………………………………………………………………………
Dotto Mwaibale
MAMLAKA ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), imetoa msaada wa madawati 100 kwa Shule ya Msingi ya Yombo iliyopo Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam   ili kukabiliana na changangamo ya madawati shuleni hapo.
Akizungumza katika hafla ya kukabidhi madawati hayo Dar es Salaam leo asubuhi Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo, Mhandisi Suleimkan Said Suleiman alisema msaada huo ni utekelezaji wa ahadi ya TAA kwa shule hiyo walioitoa mwaka jana.
“Kazi hii tunayoifanya ni kuchangia maendeleo ya jamii na Taifa na kudumisha ujirani mwema  uliopo kati ya shule yenu na Kiwanja cha chetu cha ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA)” alisema Suleiman.
Alisema mwaja jana TAA ilitoa ahadi kwa shule hiyo ya kuwapa sh.milioni 10 ili ziwezekusaidia kupunguza tatizo la madawati ahadi ambayo wameitimiza jana kwa kutoa madawati hayo yenye thamani ya sh.milioni 10.
Suleiman alisema  msaada huo utakuwa kwa kamati ya shule hiyo na kuongeza jitihada za kuboresha zaidiufaulu kwa shule hiyo na wanafunzi kuhudhuria shuleni bila ya kukosa kwa faaida yao na Taifa kwa ujumla.
Katika hatua nyingine Suleiman alitumia fursa hiyo kuuomba uongozi wa shule hiyo pamoja na wanafunzi hao kuyatunza madawati ili yaweze kusaidia na vizazi vingine.
Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Christina Kasyupa aliishukuru TAA kwa msaada huo kwa shule hiyo na kuwa wameupata kwa wakati muafaka kutokana na changamoto waliyokuwa nayo ya ukosefu wa madawati.
Shule ya Msingi ya Yombo ilianzishwa mwaka 1962 na imefanikiwa kufaulisha wanafunzi kwa asilimia 85 kwenda sekondari mwaka2013 na kupata cheti cha ugaguzi daraja A  na sasa ipo katika Mpango wa Serikali wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN) katika sekta ya elimu.

Comments