DANSI LA SERENGETI FIESTA LILIVYOCHENGUA JIJI LA TANGA

IMG_2829
Kikundi cha Platinum Dancers kikionyesha umahiri wao wakati wa shindano la kumsaka mshindi wa dansi la Serengeti fiesta, lililofanyika katika Ukumbi wa Klabu Lavida , mjini Tanga leo ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya tamasha la Serengeti fiesta linalotarajiwa kufanyika leo jumamosi Agosti 23 kwenye Uwanja wa Mkwakwani mjini humo.
IMG_2830
Majaji wa shindano la kumsaka mshindi wa  dansi la Serengeti fiesta wakifuatilia kwa makini namna wasanii wanavyotoana jasho ili kumpata mshindi wa shindano hilo.
IMG_2831
Kundi la Street Color, likionyesha umahiri wao katika  kinyang’anyiro hicho ambacho  mshindi aliondoka na kitita cha sh milioni  moja na kupata nafasi ya kutoa shoo katika tamasha la Serengeti fiesta katika Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga.
IMG_2832
Lucas Kaili wa kundi la Ice Cream naje akijaribu bahati yake wakati wa shindano hilo. 
IMG_2833
Kundi la Ice Cream likipozi kwa picha mara  baada ya kutangazwa  washindi wa dansi la Serengeti fiesta na kujishindia  zawadi ya sh milioni moja.

Comments