KATIBU MKUU WIZARA YA NISHATI NA MADINI ELIAKIM MASWI AFUNGUA SEMINA KWA MAKAMISHNA WASAIDIZI WA MADINI INAYOENDESHWA NA TANSORT BAGAMOYO
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi amefungua mafunzo yaliyoshirikisha Makamishna Wasaidizi wa Madini wa Kanda, Afisa Madini Wakazi na Wataalamu kutoka Wizara ya Nishati na Madini mjini Bagamoyo
Mkurugenzi wa Kitengo cha Uchambuzi na Uthamini wa Madini ya Almasi na Vito, (TANSORT) kilichopo chini ya Wizara ya Nishati na Madini Archard Kalugendo akiwasilisha mada kwenye semina iliyoshirikisha Makamishna Wasaidizi wa Madini wa Kanda, Afisa Madini Wakazi na Wataalamu wa Wizara ya Nishati na Madini inayoendelea Bagamoyo yenye lengo la kujadili utendaji na uboreshaji wa shughuli za uthaminishaji wa madini ya almasi na vito nchini.
Kaimu Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda ya Mashariki (kushoto) Elias Kayandabila akifuatilia kwa makini mada zilizokuwa zinawasilishwa.
Mtaalamu kutoka Kitengo cha TANSORT Teddy Goliama akisisitiza jambo wakati wa semina hiyo
Kamishna wa Madini, Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Paul Masanja akizungumza kabla ya kumkaribisha Katibu Mkuu wa Nishati na Madini Eliakim Maswi ali aweze kufungua semina hiyo
Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi akifungua semina hiyo
Baadhi ya washiriki wa semina hiyo wakifuatilia kwa makini mada zilizokuwa zinawasilishwa katika semina hiyo
Mkurugenzi wa Kitengo cha TANSORT, Archard Kalugendo (wa kwanza kushoto) Afisa Rasilimaliwatu Lameck Kabeho (katikati) na Kamishna Msaidizi wa Madini- Sehemu ya Uongezaji Thamani Mwacha Mtoro wakifuatilia kwa makini mada zilizokuwa zinawasilishwa na mtoa mada (hayupo pichani)
Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi ( wa nne kutoka kushoto waliokaa mbele) akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa semina hiyo
Mtaalamu kutoka Kitengo cha TANSORT Teddy Goliama akisisitiza jambo wakati wa semina hiyo
Mtaalamu kutoka TANSORT Edwin Rweyemamu akichangia hoja katika moja ya mada zilizowasilishwa katika semina hiyo
Comments