SHINDANO LA TANZANIA MOVIE TALENTS (TMT) LAPAMBA MOTO

Majaji wa Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) wakifuatilia Filamu fupi iliyochezwa na baadhi ya washiriki wa Shindano la Tanzania Movie talents (TMT) wakati ilipokua ikionyeshwa kwenye runinga kubwa katika Ukumbi wa Makumbusho. Kutoka Kulia ni Single Mtambalike au Rich Rich katikati ni Vyonne Cherry au Monalisa na Kushoto ni Jaji Mkuu wa Shindano hilo Roy Sarungi.
 Mahosti wa Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) Joti na Lulu wakiwajibika katika Jukwaa la Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa wakati shindano hilo lilipokuwa likiendelea alhamisi iliyopita.
 Mmoja kati ya Washindi kutoka Kanda ya Pwani, Mkoa wa Dar Es Salaam katika Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) Shiraz Ngassa (wa Kwanza Kushoto) akiongea na Msanii Joti mara baada ya Kuaga rasmi shindano hilo lililofanyika katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa siku ya alhamisi.
 Fredy Kiluswa ambae pia alikuwa mmoja kati ya Washindi watano kutoka Kanda ya Pwani katika Hatua ya kuwatafuta washindi wa Kanda akitoa maneno ya Shukrani mara baada ya kuaga shindano hilo kutokana na uchache wa kura alizopata.
 Baadhi ya washiriki wa kundi la Kwanza wakiwa mbele ya Majaji wa Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) mara baada ya Filamu yao fupi kuonyeshwa.
Mwinshehe Mohamed ambae alikua mmoja kati ya Washindi wa Tatu kutoka Kanda ya Kati mkoa wa Dodoma akitoa pongezi na Maneno ya Shukrani kwa Timu nzima ya TMT mara baada ya kuaga shindano alhamisi katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa.
 Baadhi ya washiriki wa Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) waliofanikiwa kuingia hatua ya Fainali ambapo mshindi wa Shindano hilo linalotarajiwa kufikia Tamati Mnamo mwisho wa Mwezi wa Nane kwa Mshindi Kukabidhiwa Kitita Cha Shilingi Milioni hamsini za Kitanzani.Picha Zote na Josephat Lukaza – Proin Promotions ltd

Na Josephat Lukaza – Proin Promotions Limited – Dar Es Salaam.

Hatimaye Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) limefikia hatua ya Mwisho kabisa mara baada ya washiriki kumi bora kupatikana katika Show ya Mchujo iliyofanyika katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa siku ya Alhamisi.

Show hiyo ya Mwisho katika katika Hatua ya mchujo ilifanyika siku ya Alhamisi na kupelekea Washiriki watatu kutoka Kanda Mbili za Tanzania yaani Kanda ya Kati na Kanda ya Pwani kuondolewa katika Kinyanganyiro hiko na Kupelekea Shindano hilo kubaki na washiriki 10 tu ambao wameingia hatua ya fainali ambapo mshindi mmoja ataondoka na kitita cha Shilingi Milioni 50 za kitanzania katika Fainali Kubwa inayotarajiwa kufanyika katika Ukumbi wa Mlimani City siku ya Tarehe 30 Mwezi huu wa Nane.

Washiriki waliondolewa katika Kinyanganyiro Hiko ni Mwinshehe Mohamed ambae alikuwa mmoja kati ya Washindi watatu kutoka Kanda ya Kati ambapo anafanya Idadi ya washiriki wawili kutoka Kanda ya Kati kuondolewa na Kuifanya Kanda ya Kati kuwakilishwa na Mshindi Mmoja katika Fainali hiyo. Wengine waliotoka ni Shiraz Ngassa na Fredy Kiluswa ambao wote ni Washindi kutoka kanda ya Pwani Mkoa wa Dar Es Salaam. Kanda ya Pwani walichukuliwa washindi watano huku Shiraz na Fredy wakitimiza idadi ya Washiriki wanne kuondolewa katika kinyanganyiro hiko kwa Kanda ya Pwani, Tishi Abdallah ndie Mshindi mmoja kati ya washindi watano kutoka kanda ya Pwani ambae anaiwakilisha Kanda ya Pwani katika Fainali kubwa ya Shindao la Kwanza na la Kipekee kufanyika Afrika Mashariki na Kati la Tanzania Movie Talents (TMT).

Mpaka Sasa Ni Kanda Moja tu ambayo washindi wake wote watatu ndio wanaiwakilisha Kanda hiyo katika Fainali kubwa itakayofanyika Mwishoni Mwa Mwezi wa Nane katika Ukumbi wa Mlimani city ambapo mshindi mmoja ataondoka na Kitita Cha Shilingi Milioni 50 za Kitanzania huku washindi wote kumi waliofanikiwa kuingia Katika hatua ya Fainali watakuwa chini ya Kampuni ya Proin Promotions limited ambapo watacheza filamu ya pamoja na Hatimaye kuanza kunufaika na Mauzo ya Filamu hiyo inayotarajiwa kutoka Hivi Karibu.

Vipindi vya Shindano hili la Tanzania Movie Talents (TMT) vitaendelea kurushwa katika Kituo cha Runinga cha ITV siku ya Jumamosi Saa 4 Usiku huku marudio yake yakiwa siku ya Jumapili Saa 10 Jioni na Siku ya Jumatano saa 5 usiku.

Ili Kuendelea kumuwezesha Mshiriki wako kuibuka mshindi wa Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) kwa Mwaka 2014 unachotakiwa ni kuendelea kumpigia kura kwa wingi kadri uwezavyo kwa Kuandika Ujumbe Mfupi wa Maneno (SMS) Neno TMT acha nafasi ikifuatiwa na namba ya Mshiriki halafu tuma kwenda 15678. Mfano TMT 00 halafu tuma kwenda 15678 au unaweza kupiga kura pia kupitia Ukurasa wetu wa Facebook kwa kufungua kiunganishi hiki https://www.facebook.com/tztmt/app_316963748468949

Comments