WASANII WALIOSHIRIKI TAMASHA LA KILIMANJARO MUSIC TOUR 2014 MJINI DODOMA WAMFARIJI MSANII MWENZAO AFANDE SELE KWA KUFIWA NA MKEWE

 
 Baadhi ya Wasanii waliokuwa kwenye onesho la Kilimanjaro Music Tour lililofanyika mkoani Dodoma jana, walipitia nyumbani kwa Mfalme wa Rhymes a.k.a Simba Mzee a.k.a Afande Sele kumpa mkono wa pole na kumfariji kufuatia kifo cha Mzazi mwenzake Mama Tunda kilichotokea mwisho mwa wiki mjini Morogoro. Pichani ni Msanii wa Muziki wa Bongofleva atambulikae kwa jina la Shilole akimfariji Afande Sele
 Malkia wa Taarab hapa nchini,Bi Khadija Kopa akimfariji Afande Sele, pichani nyuma ya Afande Sele ni nguli wa muziki wa Reggae hapa nchini, Innocent Nganyagwa.
 Afande Sele akifarijiwa na mkali wa hip hop katika anga ya muziki wa Bongofleva, Joh Makini
  Baadhi ya Wasanii waliokuwa kwenye onesho la Kilimanjaro Music Tour
lililofanyika mkoani Dodoma jana, wakiwa katika picha ya pamoja na Afande Sele mara baada kupitia nyumbani kwa msanii huyo na kumpa mkono wa pole na
kumfariji kufuatia kifo cha Mzazi mwenzake Mama Tunda kilichotokea
mwisho mwa wiki mjini Morogoro.
 Pichani ni mmoja Wanahabari kutoka gazeti la Mwananchi na Efm, Henry Mdimu, Joh Makini pamoja na Ben Paul wakiwa katika picha ya pamoja.
Wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumfariji Afande Sele.Picha zote kwa hisani ya Dj Choka aliyekuwepo kwenye msafara huo, Afande Sele aliwashukuru Marafiki, washabiki wake ndugu jamaa na Marafiki kwa umoja na mshikamano waliouonesha kwake katika kipindi hiki kigumu ambacho hakikuwahi kumtokea katika maisha yake ya kuondokewa na Mpendwa Mke/mzazi mwenzake. ” sina maneno yanayoweza kuelezea kwa wepesi faraja,upendo na ushirikiano nilioupata kutoka kwenu,nawashukuruni sana ndugu zangu” ,alimaliza kusema Afande sele huku akionekana kuwa mwenye simanzi kubwa

Comments