Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mama Aisha Bilal akizungumza wakati wa uzinduzi wa Sabuni ya Unga ya Omo Fast Action uliofanyika kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es salaam jana.
Meya wa Ilala Mh Jerry Silaa akimkaribisha Mke wa Makamu wa Rais Mama Aisha Bilal ili kuzungumza na wageni waalikwa katika uzinduzi huo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Unilever Afrika Mashariki na Masoko Mapya, Marc Engel akielezea malengo ya kuzindua idhaa hiyo mpya wakati wa uzinduzi huo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Unilever Afrika Mashariki na Masoko Mapya, Marc Engel akimmuonyesha zawadi Mama isha Bilal wakati wa uzinduzi huo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Unilever Afrika Mashariki na Masoko Mapya, Marc Engel.akim kabidhi zawadi mama Aisha Bilal huku Meya wa Ilala Mh. Jerry Silaa akishuhudia tukio hilo.
Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mama Aisha Bilal akiongozana na Meya wa Ilala Mh. Jerry Silaa na Mama Germina Lukuvi wakielekea katika ukumbi wa hafla uzinduzi ya uzinduzi huo kwenye hoteli ya Serena jana kushoto ni mmoja wa waratibu Teddy Mapunda Mkurugenzi wa Kampuni ya Montage
Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mama Aisha Bilal akionyesha zawadi yake aliyokabidhiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Unilever Afrika Mashariki na Masoko Mapya, Marc Engel kulia ni Meya wa Ilala Mh. Jerry Silaa na kushoto ni Meneja Masoko wa Uniliver Teresia Kamweru
Baadhi ya wageni waalikwa waliohudhuria katika hafla hiyo.
Baadhi ya warembo wakionyesha Omo kubwa katika mfuko.

Mmoja wa wasanii akionyesha jinsi sabuni ya Omo inavyotakatisha nguo.
…………………………………………………………………………
Kampuni ya Unilever Tanzania Limited, imezindua rasmi toleo jipya la sabuni yake ya kufulia ya Omo ambayo inaondoa madoa sugu haraka zaidi na kuacha nguo zikinukia vizuri. Sabuni hiyo mpya ya ‘Omo Fast Action’ imezinduliwa katika hafla iliyohudhuriwa na wageni mbalimbali akiwemo Mheshimiwa Mama Asha Bilal, mke wa Makamu wa Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wawakilishi kutoka wizara ya Ustawi wa Jamii, Jinsia na Watoto, Mstahiki Meya wa Ilala, Jerry Silaa, Wawakilishi kutoka Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Unilever Afrika Mashariki na Masoko Mapya, Marc Engel.
Akizungumza wakati wa uzinduzi, Marc Engel, Mkurugenzi Mtendaji wa Unilever Afrika Mashariki na Masoko Mapya, alisema uzinduzi huu wa sabuni ya OMO Fast Action unaileta teknolojia ya kisasa kabisa nchini, kwani OMO Fast Action mpya inaondoa madoa sugu haraka zaidi, ina manukato mazuri na yanadumu kwa muda mrefu, huku ikiiacha mikono laini na haivubazi nguo.
“Sisi Unilever tunatambua shughuli nyingi zinazowakabili wakinamama majumbani, ‘Omo Fast Action’ ndio suluhisho lao kwani sasa ina uwezo wa kusafisha nguo na zikawa safi kabisa katika kipindi cha dakika moja tu. Sabuni hii ambayo sasa inapatikana katika paketi zenye muonekano mpya, ni laini kwa mikono yako na inaacha nguo zikiwa na manukato ya kunukia vizuri” alisema Engel.
Engel pia aliwakumbusha wakinamama wasiwakataze watoto kuchafuka wanapocheza kwani wakicheza hawakusanyi uchafu peke yake bali pia ndio wanajifunza na kugundua vitu mbalimbali vinavyowazunguka. Kama kauli mbiu ya OMO inavyosema, ‘Uchafu ni Mzuri’, kinamama wa kitanzania sasa wanaweza kuwapa watoto uhuru wa kucheza na kujifunza bila kuwa na wasiwasi wa nguo kubaki na madoa sugu baada ya kufuliwa.
Naye mgeni rasmi wa uzinduzi huo, Mheshimiwa Mama Asha Bilal aliipongeza kampuni ya Unilever kwa jitihada zao katika kuboresha maisha ya kinamama na watoto siku hadi siku.
Mama Bilal pia alipongeza uboreshaji wa sabuni ya Omo kwa kuwawezesha kinamama kufua kwa muda mfupi sana na hivyo kupata nafasi kushiriki katika shughuli za maendeleo. “Katika ulimwengu wa sasa, mwanamke hakai nyumbani tu kama golikipa, mwanamke anapaswa kushiriki katika shughuli za kiuchumi ili kusaidia kuongeza pato la familia. Mimi kama mama, naelewa kuna changamoto nyingi za majukumu ya familia, lakini nahamasisha kinamama kote nchini, tuamke, tupambane, ili kuimarisha nafasi yetu katika familia na jamii yetu kiujumla.”
No comments:
Post a Comment