Wednesday, August 27, 2014

SERIKALI YAKABIDHIWA MAGARI NA PIKIPIKI KUTOKA SHIRIKA LISILO LA KISERIKALI LA UJERUMANI (GLRA) KWA AJILI YA MPANGO WA TAIFA WA KUDHIBITI UGONJWA WA KIFUA KIKUU NA UKOMA

Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk.Seif Rashid akizungumza na waandishi wa habari wakati akipokea magari hayo Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Charles Palanjo akizungumza na katika hafla hiyo. (Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com-namba ya simu 0712-727062)
.
Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Wahisani la Kijerumani linalohudumia Ukoma na Kifua Kikuu (GLRA), Burchard Rwamtoga, akisoma risala kabla ya kukabidhi msaada huo.
Mganga Mkuu wa Serikali Donan Mmbando (kulia), akimkalibisha Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk.Seif Rashid (katikati), kuzungumza na wadau wa sekta ya afya na wanahabari wakati wa kupokea msaada huo. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Charles Palanjo.
Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Wahisani la Kijerumani linalohudumia Ukoma na Kifua Kikuu (GLRA), Burchard Rwamtoga (wa pili kushoto), akimkabidhi  Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk.Seif Rashid (kulia),moja ya ufunguo wa gari kati ya magari manne na pikipiki 20 vyote vikiwa na thamani ya sh.261,105,615, Dar es Salaam leo, zilizotolewa na shirika hilo kwa Serikali ya Tanzania kwa ajili ya kupambana na magonjwa hayo nchini. Wanashuhudia kutoka kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Charles Palanjo na Naibu Waziri, Dk. Steven Kebwe.
Naibu Waziri, Dk. Steven Kebwe (wa pili kulia), na viongozi wengine wa wizara hiyo wakiwa kwenye hafla hiyo. Kutoka kulia ni Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Charles Palanjo, Mganga Mkuu wa Serikali Donan Mmbando na Mkurugenzi Msaidizi Afya na Usafi wa Mazingira, Elias Chinamo.
Pikipiki zilizotolewa kwa serikali.
Magari yaliyotolewa kwa Serikali.

Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Wahisani la Kijerumani linalohudumia Ukoma na Kifua Kikuu (GLRA), Burchard Rwamtoga, akisoma risala kabla ya kukabidhi msaada huo. Kutoka kushoto ni Mganga Mkuu wa Serikali, Donan Mmbando, Meneja wa Ofisi ya Uhasibu wa GLRA, Lucy Mgoba na Mshauri wa Tiba wa GLRA, Blasdus Njako.
Wadau wa Sekta ya Afya wakiwa kwenye hafla ya kupokea msaada huo.
Wanahabari wakiwa kwenye sherehe hiyo.
Wadau wa sekta ya afya na wanahabari wakiwa kwenye sherehe hiyo.
Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Wahisani la Kijerumani linalohudumia Ukoma na Kifua Kikuu (GLRA), Burchard Rwamtoga (kushoto),akiwa kwenye hafla hiyo na wenzake. Kulia ni Mshauri wa Tiba wa GLRA, Blasdus Njako na  Meneja wa Ofisi ya Uhasibu wa GLRA, Lucy Mgoba.
Wadau wa Sekta ya Afya wakiwa kwenye hafla hiyo. Kutoka kulia ni Mkurugenzi Msaidizi Afya na Usafi wa Mazingira, Elias Chinamo, Naibu Meneja kutoka WTCP, Dk.Liberate Mleoh na Meneja Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Kifua Kikuu na Ukoma, Dk.Beatrice Mutayoba.
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk.Seif Rashid (kulia), akimkabidhi ufunguo wa gari Mratibu wa Huduma za Kifua Kikuu na Ukoma wa Mkoa wa Dk. Deus Leonard katika hafla hiyo.
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk.Seif Rashid akijaribu kuwasha moja ya magari hayo.
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk.Seif Rashid(kulia), akimkabidhi ufunguo wa gari Mratibu wa Huduma za Kifua Kikuu na Ukoma wa Mkoa wa Kitabibu wa Ilala, Dk.Mbarouk Seif.
Dotto Mwaibale

SERIKALI imepokea msaada wa magari manne na pikipiki 20 zenye thamani ya sh. 
.261,105,615 kutoka Shirika la Wahisani la Kijerumani linalohudumia Ukoma na Kifua Kikuu (GLRA) kwa ajili ya kusaidia sekta ya afya.
Akipokea msaada huo Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid alisema Tanzania imefikia lengo la kimataifa la kutokomeza ukoma kwa kuwa chini ya mgonjwa mmoja katika watu 10,000 hivyo kufanya ukoma kutokuwa tatizo kubwa la afya nchini.Alisema pamoja na kupokea msaada huo bado kumekuwa na changamoto ikiwemo za ukosefu wa magari na pikipiki kwa mikoa na wilaya mpya ambapo Serikali kupitia mpango huo unafanya jitihada za kupata vyombo vya usafiri katika mikoa hiyo.
Alisema vyombo hivyo vya usafiri vitapelekwa katika mikoa ya Kigoma, Tanga, Halmashauri za Ilala na Kinondoni ambapo aliomba  vitumika vizuri kulingana na malengo yaliyokusudiwa.
“Napenda kuuwaasa waganga wakuu wa mikoa na wilaya kusimamia kikamilifu matumizi ya vyombo hivi vya usafiri kwa kuhakikisha wale wote watakaokabidhiwa wanavilinda kwa kuvitumia vizuri kulingana na malengo yaliyokusudiwa na kwa kufuata taratibu za serikali na si vinginevyo,” alionya.
Dk. Rashid alitoa wito kwa Halmashauri zote nchini kuangalia namna ya kuchangia gharama za matengenezo ya vyombo hivyo ili kuziba pengo la kupungua kwa misaada inayotolewa na wahisani.

No comments: