MAKATIBU UENEZI WA CCM WA KATA 90 MKOA WA DAR ES SALAAM WAPATIWA SEMINA ELEKEZI

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida (katikati), akizungumza na makatibu waenezi 90 wa CCM wakati akifungua semina elekezi ya siku moja kwa makatibu hao kutoka Kata mbalimbali za mkoa wa Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu Muenezi wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Juma Simba na Katibu Muenezi Msaidizi wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Athuman Salum.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida (katikati), akizungumza na makatibu hao.
Makatibu Uenezi hao wakishangilia hutuba ya mgeni rasmi, Ramadhani Madabida.
Makatibu Uenezi kutoka Wilaya ya Kinondoni wakiwa kwenye semina hiyo.
Makatibu Uenezi kutoka Wilaya ya Temeke wakiwa kwenye semina hiyo.
Makatibu Uenezi kutoka Wilaya ya Ilala wakipitia taarifa yao ya utekelezaji wa Ilani ya CCM na uhai wa chama chao.
Makatibu uenezi wa Wilaya ya Ilala wakiwa kwenye semina hiyo.
Hapa makatibu hao wakiwa kwenye majadiliano.
Makatibu hao kutoka Wilaya ya Temeke wakifuatilia kwa makini hutuba ya mgeni Rasmi Ramadhani Madabida.
Makatibu uenezi hao wakiwa kwenye semina hiyo. Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)
 
Dotto Mwaibale
 
MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida amewataka makatibu waenezi wa chama hicho kumtetea Rais Jakaya Kikwete na chama hicho ili aendelee kuaminiwa na wananchi.
 
Madabida alitoa mwito huo wakati akifungua semina elekezi ya siku moja iliyoandaliwa mahususi kwa makatibu waenezi 90 wa chama hicho kutoka kata mbalimbali za mkoa wa Dar es Salaam iliyofanyika jana ofisi ya CCM Wilaya ya Ilala.
 
“Ninyi ni kama maofisa mawasiliano na masoko hivyo mnawajibu wa kukiuza na kukitangaza chama chetu kwa wananchi ili waendelee kuwa na imani nacho na serikali kwa ujumla” alisema Madabida.
 
Alisema kazi yenu kubwa ni kumtetea rais ambaye ni Mwenyekiti wetu wa chama taifa na ili aendelee kuheshimika kwa wananchi hasa pale anapochafuliwa na wapinzani.
 
Katika hatua nyingine Madabida aliwataka makatibu ueneze hao kuwa wamoja na kuacha kuwachukia viongozi waliopo madaraka baada ya chaguzi kuisha na akatoa onyo kuwa hata kuwa na mswalia mtume kwa mtu atakayebainika kuendeleza chuki hicho.
 
“Kumekuwa na tabia ya watu kuendeleza chuki baada ya kukosa nafasi katika uchaguzi hivyo kutufanya tushindwe kusonga mbele nasema katika hilo mtaniita majina mengi mabaya kwani siqwezi kumvumilia mtu” aliongeza Madabida.
 
Madabida aliwataka makatibu uenezi hao kufanya mikutano ya hadhara ili kukinadi chama chao kwani wenye wajibu wa kutekeleza ilani ya chama ni wao na si mtu mwingine.

Comments