OFISI YA CHADEMA KATA YA RUAHA JIMBO LA IRINGA MJINI YACHUKULIWA NA CCM BAADA YA CHADEMA KUSHINDWA KULIPA KODI

IMG_9966Katibu wa CCM kata ya Ruaha Rashid Shungu ( wa  pili  kushoto ) na kada wa Chadema aliyehamia CCM Ibrahim Mmasi  pamoja na  wanachama  wengine wa CCM wakiwa  wameshika bendera ya CCM ambayo itapepea katika ofisi mpya ya kata ya Ruaha ,ofisi ambayo awali ilikuwa ikimilikiwa na Chadema kabla ya  kufukuzwa kwa  kushindwa kulipa deni la kodi kiasi cha Tsh 540,000 , kushoto fundi rangi akiendelea  kupaka rangi ya CCM
IMG_9940Fundi akipaka rangi kuta za ofizi hiyo 
……………………………………………………………….. 
CHAMA  cha  demokrasia na maendeleo (CHADEMA) kata ya Ruaha  jimbo la Iringa  mjini kimepata  pigo  kubwa baada ya kufukuzwa katika nyumba  waliyopanga kama ofisi  ya kata  hiyo baada ya  kushindwa  kulipa deni la  pango  kiasi cha Tsh 540,000 walizokuwa  wakidaiwa na mwenye nyumba  deni  ambalo limelipwa  na Chama  cha mapinduzi (CCM ) kata ya  Ruahakabla ya  kuichukua ofisi  hiyo .
 
Mmiliki  wa nyumba  hiyo iliyopo mtaa wa Ngeleli Ipogolo Bi  Neema Mwasika alifikia  hatua  hiyo ya  kuwataka  kuondoka katika  ofisi  hiyo baada ya  jitihada za  kudai  deni lake  kushindikana na  hivyo kulazimika  kupangisha nyumba   hiyo yenye  chumba  kimoja na sebure  kwa  mpangaji mpya ambae ni CCM kata ya Ruaha.
 
Akizungumza na waandishi  wa habari  leo katibu  wa  CCM kata ya Ruaha Rashid Shungu alisema  kuwa  awali CCM  kilikuwa na ofisi  yake  eneo la Ruaha  jirani na mto hivyo  kutokana na mvua  kubwa  zilizonyesha mwaka jana  zilipelekea  ofisi hiyo  kuharibiwa  vibaya na  hivyo  kukosa kabisa  ofisi .
 
Alisema kuwa  kutokana na kutokuwa na ofisi  cham a kilikuwa  kikitumia nyumba ya mtu binafsi kama  ofisi  pale ilipohitajika  kukutana  viongozi ama wanachama  .
 
Shungu alisema  kuwa jitihada za  kutafuta  nyumba ya  kupanga  ili  kutumika kama  ofisi ya muda ya  CCM kata  hiyo ya  Ruaha  ziliendelea kufanyika  chini ya aliyekuwa kada wa Chadema kata  hiyo kabla ya  kujiunga na CCM Bw  Ibrahim Mmasi
 
Hata  hivyo  alisema ofisi  hiyo alisema kuwa baada ya  kuona  ofisi  hiyo imefungwa kwa  muda na kuwasiliana na mwenye nyumba alikubali  kuwapangisha kwa makubaliano ya  kulipa deni kwanza jambo ambalo  lilifanyika  hivyo na kulipia kodi ya miaka  miwili zaidi.
 
” Tumeipata  ofisi  hii kihalali na sio hujuma kwani  makubaliano  kati ya mmiliki wa nyumba na mpangaji yalifanyika na  hivyo kwa  kuwa  hitaji letu  nyumba ya kupanga  tuliona  hiyo  ina  sifa ambayo tuliitaka  hivyo  tunachofanya ni kufuta rangi na nembo  za Chadema na kuweka rangi ya CCM na nembo  zetu …..na tutaizindua rasmi jumapili  wiki  hii”
 
Kwa upande wake  kada   wa CCM aliyehama kutoka Chadema Bw Mmasi  alisema  kuwa ofisi hiyo  ilikuwa imezinduliwa na viongozi wa  kitaifa  kupitia zoezi la oparesheni Sangara tarehe 19 mey 2011 chini ya  naibu mkuu wa Chadema enzi hizo Zitto Kabwe na mbunge wa  jimbo la Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa na viongozi  wengine .

Comments