Saturday, August 23, 2014

AIRTEL MONEY YAZINDUA RASMI HUDUMA YA KUTUMA NA KUPOKEA PESA MOJA KWA MOJA KWENYE AKAUNTI YA TIGO PESA

DSC_0056
Mkurugenzi mtendaji wa Airtel Bwana Sunil Colasa akiongea na waandishi wa habari leo hii (hawapo pichani) akiwatangazia kuanza kutumika rasmi kwa huduma mpya ya kutuma na kupokea pesa kutoka kwenye mitandao mingine moja kwa moja kwenye akaunti  zao za Airtel money, (interoperability) huduma hii ni ya kwanza Duniani ambapo inaaminika kuwa itasaidia sana wateja wa Airtel Money na Wakala kuokoa muda wa kupata na kutoa huduma kwa haraka Zaidi.
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imezindua huduma itakayowawezesha wateja wake wa huduma ya Airtel Money kutuma na kupokea pesa kutoka kwenye mitandao mingine moja kwa moja kwenye akaunti  zao za Airtel money ,  huduma hii ni ya kwanza Afrika na duniani kwa ujumla na hivyo inaweka historia nchini kuzinduliwa ya kwanza kupitia njia ya  mtandao wa simu.
Huduma hii ya kwanza Duniani na Afrika inayohusisha makampuni ya simu Airtel na Tigo ulitangazwa kuwa itaanza kutumika mwishoni mwa mwezi wa Julai na sasa iko tayari ambapo wateja wa Airtel Money  wataweza kutumia  huduma hii kabambe na yenye utofauti kwa inaaminika kuwa ni  rahisi zaidi, salama na ina unafuu katika kutuma pesa kwa kutoka mteja mmoja kwenda mwingine na kuingia moja kwa moja katika (e-wallet) akaunti yake ya simu/mtandao anaotumia na kuweza kuitoa popote alipo.
Akiongea wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo Mkurugenzi wa Airtel Bwana Sunil Colaso alisema” Tunayofuraha kushirikiana na makampuni mengine ya simu katika kuhakikisha tunaendelea kutoa huduma za kisasa, zenye ubunifu na kwa gharama nafuu. Ushirikiano huu utawawezesha wateja wa Airtel kutuma na kutoa pesa kutoka kwenye mitandao mingine .  sasa wateja wetu watapokea pesa kutoka kwenye mitandao mingine na kuingia moja kwa moja kwenye (e-wallet) akaunti  zao za Airtel money hivyo kuondoa usumbufu ulikuwepo awali  ambapo mteja anapotumiwa pesa kutoka mtandao mwingine alitakiwa kuzitoa ndani ya siku 7.
Kwa uzinduzi huu  leo tunafanya huduma hii ya kifedha kwa njia ya mtandao kukidhi mahitaji ya wateja.
Vile vile mawakala wetu pia wamerahisishiwa utoaji huduma  ambapo sasa hakutakuwa na haja ya wakala kupata udhibitisho wa ujumbe kutoka kwa simu ya mteja kabla ya kufanya malipo.  Tunaamini huduma hii itaongeza usalama wa mawakala na wateja nchini, Pia itamuongezea wakala muda wa kuhudumia wateja wengi Zaidi kwa uhakika, haya ni mapinduzi ya huduma za kifedha ambayo tunaamini ni maendelea makubwa ya maboresho ya huduma hii aliongeza kwa kusema Colaso
Akiongea kuhusu huduma hiyo mmoja wa wakala ambae alijaribu wa Airtel Money Pasco Woiso alisema “Tunafurahia huduma iliyoanzishwa na Airtel kwa kushirikiana  na mitandao mingine,  leo nimeitumia huduma hii kwa mara ya kwanza lakini nimefurahishwa na ufanisi wake na jinsi wateja wanavyoipokea vizuri nikiwapasha habari kuhusu huduma hiii.  Kwa sisi wakala awali tulikuwa na tatizo la kupata ujumbe wa malipo, kitambulisho cha malipo na pesa kurudi baada ya muda wa siku saba,  lakini kwa sasa ushirikiano huu umeifanya huduma hii ya pesa kwa mtandao kuwa bora zaidi na kupunguza muda niliokuwa nautumia kumuhudumia mteja moja na hivyo

No comments: