Na Magreth Kinabo
Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Samuel Sitta amewahakikishia Watanzania kwamba Katiba Mpya itakayopatikana itakuwa imezingatia matakwa ya makundi mbalimbali.
Mhe . Sitta aliyataja makundi hayo baadhi ya makundi hayo kuwa ni wafugaji, wakulima, wavuvi na wasanii.Huku akisema Katiba Mpya itakayopatikana itakuwa ni bora kuliko iliyopo sasa.
Kauli hiyo ilitolewa jana na Mhe . Sitta wakati akizungumza na wafugaji wapato 44 kutoka mikoa mbalimbali,ambao waliongozwa na Mwenyekiti wa ujumbe huo, Huruma Ole Kalaita na Mlezi wao, ambaye mjumbe wa Bunge hilo na Mbunge wa Jimbo la Maswa Magharibi(CHADEMA).
“Tunaamini ni wakati wa Katiba Mpya… lazima iweze kupatikana. Itakayozingatia Sheria bora na maslahi ya makundi mbalimbali yatapatikana.
“ Utungaji wa Katiba ni suala la wananchi kutanguliza suala la muundo wa Serikali si haki. Ni muhimu kutanguliza haki za raia. Kinachotangulia ni haki za raia wetu na makundi mbalimbali,” alisisitiza Mhe. Sitta.
Aidha Mhe. Sitta aliwakikishia wafugaji hao,kwamba Bunge hilo “ liko hapa kisheria kwa kanuni zake linaendelea na wale wanaopiga kelele hawalitakii mema taifa letu kwa sababu demokrasia yoyote ni kupata kura ya walio wengiu,” alisema.
Kwa upande wake Mlezi wa wafugaji hao, Mhe. Shibuda alimpongeza Mhe. Sitta kwa jitihada zake za kuendeleza vikao vya Bunge hilo, ambapo pia alimsihii kuwa asikatishwe tamaa kwa dhamira yake njema ya kuendelea kuongoza vikao vya Bunge hilo.
Akizungumzia kuhusu masuala ya wafugaji hao na wakulima wa zao la pamba nchini, alisema kuwa wako pamoja naye.
“ Hivi Serikali tatu au mbili inatiririsha nini kwa wakulima na wafugaji. Tunataka viongozi wa kukabiliana na matatizo ya wananchi,” alisisitiza Shibuda.
Kwa upande Mwenyekiti wa wafugaji hao, Kalaita alipendekeza Katiba Mpya, itamke matumizi bora ya ardhi kati ya wakulima na wafugaji ili kuondoa migogoro ya wakulima na wafugaji.
Makamu wa Mwenyekiti wa wafugaji hao, Kasundwa Wamalwa kutoka Kanda ya Magharibi akisoma mapaendekezo ya risala yao waliyoiwasilisha kwa Mwenyekiti wa Bunge hilo, Mhe. Sitta, ambapo walipendekeza Katiba Mpya itambue wafugaji wa asili.
Aidha Makamu Mwenyekiti huyo aliwataka wajumbe wa Bunge hilo, kuwa na hofu ya Mwenyezi Mungu wakati wanapoendelea na mchakato huo.
Miongoni mwa makundi mengine waliofika katika ofisi za Bunge mjini Dodoma ni Jukwaa la Katiba (JUWAKATA) na Jukwaa la Wahariri.
Comments