KIKWETE: SERIKALI HAINA MAMLAKA YA AMRI KUZUNGUMZIA URAIA PACHA

IMG_9796
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mkrisho
Kikwete akiingia ukumbini wakati wa kongamano la Watanzania waishio
Ughaibuni lililofanyika kwa mara ya kwanza nchini jana Jijini Dar es Salaam.
Nyuma yake ni Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizendo
Pinda( mwenye koti la Bluu). Hassan Silayo-MAELEZO
IMG_9810(1)
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Watanzania waishio Nje ya Nchi Bw.
Emannuel Mwachulla akitoa shukrani kwa Serikali ya Tanzania kwa mchango
wake katika masuala ya kuwadhamini watanzania waishio Ughaibuni, wakati wa
kongamano la Watanzania waishio nje ya Nchi lililofanyika kwa mara ya kwanza
nchini jana Jijini Dar es Salaam.
IMG_9842
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizendo Pinda
akiwaeleza jambo Watanzania waishio Ughaibuni wakati wa kongamano la
Watanzania waishio ughaibuni lililofanyika kwa mara ya kwanza nchini jana Jijini
Dar es Salaam.
IMG_9895
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mkrisho
Kikwete akiwaeleza jambo Watanzania waishio Ughaibuni na kusisitiza kuhusu
wajibu wao wa kukumbuka nyumbani na kuendelea kuchangia katika masuala la
uchumi na kijamii kwa ujumla kwa ajili ya maendeleo ya nchi
IMG_9921
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizendo Pinda
akimueleza jambo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya
Mkrisho Kikwete wakati wa kongamano la Watanzania waishio ughaibuni
lililofanyika kwa mara ya kwanza nchini, jana Jijini Dar es Salaam.
IMG_9926
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mkrisho
Kikwete akiangalia tovuti ya Umoja wa Watanzania waishio nje ya baada ya
kuizindua tovuti hiyo jana jijini Dar es Salaam.
IMG_9929
Mbunge wa viti maalum kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(CHADEMA) Leticia Nyerere (Kushoto) akiteta jambo na Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mkrisho Kikwete wakati wa kongamano la
Watanzania waishio ughaibuni lililofanyika kwa mara ya kwanza nchini, jana Jijini
IMG_9934
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Dkt. Jakaya Mkrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na watanzania
waishio Ughaibuni wakati wa kongamano la Watanzania waishio ughaibuni
lililofanyika kwa mara ya kwanza nchini, jana Jijini Dar es Salaam.
IMG_9940
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Dkt. Jakaya Mkrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na watanzania
waishio Ughaibuni wakati wa kongamano la Watanzania waishio ughaibuni
lililofanyika kwa mara ya kwanza nchini, jana Jijini Dar es Salaam.
…………………………………………………………………………….
Na Joseph Ishengoma
MAELEZO
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Mrisho Kikwete amesema
hana mamlaka ya amri kuzungumzia uraia pacha kwasababu ni la katiba.
Rais Kikwete amesema hayo leo katika kongamano la kwanza la diaspora
lililofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar Es Salaam. Diaspora ni lugha
inayotumika kuwatambulisha Watanzania walioko nje ya nchi wanaojiendeleza
kwa njia mbalimbali ikiwemo elimu.
Kongamano hilo la siku mbili lenye lengo la kuelimishana, kubadilishana mawazo
na kujadili fursa za uwekezaji, linaudhuriwa na wajumbe kutoka nchi 17 duniani.
“Serikali imelisikia suala la uraia pacha, lakini ni la kikatiba sio la Rais. Katiba
ndio sheria mama sisi hatuna mamlaka ya amri kulizungumzia.”
Kwa mujibu wa Rais, watanzania waliowengi uraia pacha hauwakeleketi, hivyo
diaspora wanaoishi nje ndio wanaostahili kulisukuma, lakini kwa sasa sauti
yao bado haijasikika sana, badala ya kulizungumzia kwa nguvu, wanatumia
muda mwingi kuzungumzia siasa za mitaani kwenye mitandao ya kijamii pindi
wanapopata nafasi.
“Sauti yenu haijasikika sana, badala yake mnatumia muda mwingi kuzungumzia
siasa za mitaani. Suala la uraia pacha liko mikononi mwa Bunge Maalum la
Katiba. Kama katiba haijasema nyinyi ni rais, sheria ikitungwa haiwezi kuwapa
uraia,” amesema.
Kwa mujibu wa Rais, rasmu ya Katiba iliyopo inazungumzia hadhi ya Watanzania
walioko nje sio uraia. “Mnachoweza kufanya ni kushawishi wabunge wa Bunge
Maalum la Katiba kukubali uraia pacha kuwa ndani ya katiba na hili sio jambo
haramu, zungumzeni nao serikali haina tatizo nalo iwapo Katiba itawatambua.”
Pamoja na uraia pacha, Rais amewaomba wanadiaspora kuzingatia uwekezaji
ndani ya nchi ili kuleta maendeleo ya kiuchumi, kutafuta masoko ya bidhaa ya
bidhaa za Tanzania nje ya nchi, kuunda umoja utakaowaunganisha na kutumia
teknolojia na maalifa wanayopata nje kuendeleza taifa lao.
Kauli mbiu ya kongamano hilo ni, “Nyumbani ni Nyumbani.”
Awali Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano Mhe. Mizengo kayanza Pinda
ametaka mkutano huo kusaidia kukata kiu ya Watanzania kupata majibu ya mambo
ambayo wamekuwa wakiulizia pindi wanapokutana na viongozi mbalimbali wan
chi nje ya Tanzania.

Comments