Saturday, August 23, 2014

PINDA AONGOZA WAOMBOLEZAJI KUTOA HESHIMA ZA MWISHO KWA JAJI MAKAME

PG4A2667
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimian na Mawaziri Wakuu, Wastaafu, Frederick Sumaye na Jaji Joseph Warioba (wapili kulia)  kabla ya kuzungumza kwa niaba ya serikali na  kutoa heshima za mwisho kwa Mwenyekiti Mstaafu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi,  marehemu Jaji Lewis Makame kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam August 22, 2014. Kulia nI jaji Mkuu wa Tanzania, Mohamed  Chande Othman. Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) PG4A2677
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda  akisalimiana na jaji Mkuu Mohamed Chande  Othman  (kulia) na Mawaziri Wakuu Wastaafu, Joseph Warioba (wapili kulia) na Frederick  Sumaye kabla ya kutoa salamu za Serikali na  heshima za mwisho kwa Mwenyekiti Mstaafu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, marehemu Jaji Lewis Makame kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam August 22, 2014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
PG4A2689
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akimpa pole Jaji Leila Makame Mgonya mmoja wa wana familia, wa  Mwenyekiti Mstaafu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi,Marehemu Jaji Lewis Makame  baada ya kuzungumza kwa niaba ya serikali na kutoa heshima za mwisho kwa marehemu huyo kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam August 22, 2014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 PG4A2702
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akitoa heshima za mwisho kwa Mwenyekiti Mstaafu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Marehemu Jaji Lewis  Makame baada ya kuzungumza kwa niaba ya serikali kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam August 22, 2014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)  PG4A2705


No comments: