LHRC, WASANII KUZINDUA FILAMU NA WIMBO WA KATIBA KWA AJILI YA KUHAMASISHA MCHAKATO WA KATIBA MPYA AGOSTI 9,2014
Kaimu Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Harold Sungusia (katikati), akionesha Rasimu ya Katiba Mpya wakati akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam, kuhusu uzinduzi wa Filamu, Wimbo wa Katiba na mpango wa kugawa Rasimu ya pili ya Katiba katika mikoa 20 ya Tanzania. Kulia ni Msanii, Chrispiny Masele na Edson Kalokola. Wasanii hao wameshiriki katika Filamu hiyo ambayo ilizinduliwa jana ukumbi wa Mlimani City.
Hapa Harold Sungusia akionesha Kadi zenye Filamu hiyo.
Msanii Edson Kalokola akizungumza kwenye mkutano huo. Kushoto ni Msanii Edwardo Mwanisongole.
Wanahabari wakiangalia filamu hiyo wakati wa mkutano huo.
Wasanii walioshiriki kucheza filamu hiyo wakiwa kwenye mkutano huo.
Wanahabari wakiwa kwenye mkutano huo.
Dotto Mwaibale
WANATAALUMA na Wasanii wametakiwa kutumia ujuzi wao ili kuelimisha jamii katika uelewa wa mchakato wa Katiba Mpya unaoendelea nchini.
Mwito huo umetolewa na Kaimu Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Halord Sungusia wakati akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana kuhusu uzinduzi wa Filamu, Wimbo wa Katiba na mpango wa kugawa Rasimu ya pili ya Katiba katika mikoa 20 ya Tanzania.
“Tunawaomba wanataaluma, wasanii watumie nafasi na vipaji walivyonavyo kuongeza hamasa ya wananchi ili washiriki kikamilifu katika mchakato wa kujipatia Katiba Mpya” alisema Sungusia.
Sungusia alisema LHRC kinaamini kuwa ni wajibu kwa vyombo vya habari kuhakikisha kwamba filamu na wimbo wa katiba vinatangazwa ili wananchi wapate elimu na taarifa sahihi ya katiba na hatimaye waweze kushiriki vyema wakati wa kupiga kura ya maoni.
Alisema hatua hiyo itahakikisha kuwa wananchi ambao ndio wadau wakubwa watapata naaaaafasi ya kushiriki kikamilifu katika safari nzima ya kupata katiba mpya na iliyo bora.
Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), kwa kushirikiana na asasi mbalimbali pamoja na wasanii wameandaa Filamu na wimbo wa katika kwa ajili ya kutoa elimu kwa wananchi kuhusu mchakato wa Katiba mpya ambapo jana Filamu hiyo itazinduliwa ukumbi wa Mlima City jijini Dar es Salaam.
Comments