Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza katika harambee ya kuchangia Mradi wa Mkapa Fellows kwenye hoteli ya JB Belmont jijini Mwanza August 23, 2014. Zaidi ya sh. Bilioni 1.3 zilichangwa. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akipokea mchango wa shilingi milioni 15 kutoka kwa Mfanyabiashara wa Mwanza na Dar es salaam Jumanne Kishimba katika harambee ya kuchangia Mradi wa Mkapa Fellows iliyofanyiak kwenye hoteli ya JB Belmont jijini Mwanza August 23,2014. Zaidi ya Shilingi Bilioni 1.3 zilichangwa. (picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa akimshukuru Mfanyabiashara wa Dar es salaam na Mwanza, Jumanne Kishimba ambaye alichangia Shilingi milioni 15 katika harambee ya kuchangia mradi wa Mkapa Felllows kwenye hotel ya JB Belmont jijini Mwanza August 23, 2014. Zaidi ya Shilingi Bilioni 1.5 zilichangwa. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Mkapa HIV/AIDS, Balozi Charles Sanga.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mmuu, Mizengo Pinda akipokea kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Kanal Fabian Massawe Maarufu kwa jina la Mulokozi mchango wa zaidi ya shilingi milioni 100 zilizochangwa na Wanakagera katika harambee ya kuchangisha fedha kwa ajili ya Mradi wa Mkapa Fellows, kwenye hoteli ya JB Belmont jijini Mwanza August 23, 2014. Zaidi ya Shilingi Bilioni1.3 zilichangwa katika harambee hiyo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu,Mizengo Pinda akipokea mchango wa zaidi ya shilingi milioni 100 kutoka kwa Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Ali Rufunga zilizotolewa na wanashinyanga kuchangia mradi wa Mkapa Fellows katika harambee iliyoongozwa na Waziri Mkuu kwenye hoteli ya JB Belmont jijini Mwanza August 23, 2014. Zaidi ya shilingi Bilioni 1.3 zilichangwa. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akimshukuru Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhandisi Evarest Ndikilo ambaye aliwasilisha mchango wa zaidi ya Shilingi milioni 100 zilizochangwa na Wanamwanza katika harambee ya kuchangia Mradi wa Mkapa Fellows iliyofanyika kwenye hoteli ya JB Belmont jijini Mwanza, August 23, 2014. Zaidi ya Shilingi Bilioni 1.3 zilichangwa katika harambee hiyo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Comments