Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na mkuu wa majeshi wa kwanza Mzalendo Jenerali Mirisho Sarakikya muda mfupi baada ya kuwasili katika chuo cha jeshi Monduli tayari kwa kutunuku kamisheni kwa maofisa 179 wapya wa jeshi waliohitimu vyema mafunzo yao mwishoni mwa wiki.
Mkuu wa Majeshi ya ulinzi na usalama Jenerali Davis Mwamunyange kushoto na Mkuu wa Chuo cha Jeshi (TMA) Monduli Brigedia Jenerali Paul Peter Massao(kulia) wakimsindikiza Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt.Jakaya Mrisho kwenda uwanja wa Paredi ambapo alitunuku kamisheni kwa maofisa wapya wa jeshi katika sherehe zilizofanyika katika chuo cha jeshi(TMA) mkoani Arusha.
Mkuu wa Chuo Cha Jeshi Monduli TMA Brigedia Jenerali Paul Peter Massao akimsindikiza Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kuingia katika viwanja vya Paredi chuoni hapo akiwa katika gari maalumu ambapo alitunuku kamisheni kwa maofisa wapya wa Jeshi.
Mkuu wa Chuo Cha Jeshi Monduli TMA Brigedia Jenerali Paul Peter Massao akimsindikiza Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kuingia katika viwanja vya Paredi chuoni hapo akiwa katika gari maalumu ambapo alitunuku kamisheni kwa maofisa wapya wa Jeshi.
Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akipokea salamu ya heshima mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Paredi kutunuku kamisheni katika chuo cha jeshi Monduli mkoani Arusha Jumamosi.
Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikagua vikosi hkwenye uwanja wa Paredi la kutunuku kamisheni katika chuo cha jeshi Monduli mkoani Arusha Jumamosi.
Maofisa Wapya wa jeshi wakipita mbele ya mgeni Rasmi Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na kutoa heshima wakati wa gwaride maalumu la Kamisheni lilofanyika katika chuo cha TMA Monduli.
Kikosi cha Bendera kikipita mbele ya Amiri jeshi mkuu Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa gwaride maalumu la Kamisheni lilofanyika katika chuo cha TMA Monduli.
Maofisa Wapya wa jeshi wakipita mbele ya mgeni Rasmi Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete nakutoa heshima wakati wa gwaride maalumu la Kamisheni lilofanyika katika chuo cha TMA Monduli.
Comments