Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa King’ongo, Demetrius Mapesi (kulia),akimtwisha ndoo ya maji Radhia Said baada ya kuzindua mradi wa kisima cha maji mwishoni mwa wiki kilichojengwa kwa msaada wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) katika Kata ya King’ongo, wilayani Kinondoni, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Kisima hicho kimejengwa kwa msaada wa TBL. Kushoto ni Meneja Mauzo wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Kanda ya Kinondoni, Joseph Nicholaus
Meneja Mauzo wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Kanda ya Kinondoni, Joseph Nicholaus (kushoto) na Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa King’ongo, Demetrius Mapesi wakifunua pazia ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa kisika cha maji kiolichojengwa kwa gharama ya sh. mil. 29 kwa msaada wa TBL katika Kata ya King’ongo, wilayani Kinondoni, Dar es Salaam. Wanaopiga makofi ni wananchi wa eneo hilo wakionekana kufurahishwa na msaada huo muhimu kwani wataondokana na tatizo la maji ambapo walikuwa wakitembea zaidi ya KM 2 kununua maji ndoo moja sh. 700. Katika Kisima hicho watakuwa wananunua ndoo moja ya maji kwa sh. 50.
Meneja Mauzo wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Kanda ya Kinondoni, Joseph Nicholaus, akifungua maji kwenye bomba lililounganishwa kwenye kisima hicho. Kisima hicho kina uwezo wa kutoa zaidi ya lita 5000 za maji kwa saa. PICHA ZOTE NA KAMANDA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
Meneja Mauzo wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Kanda ya Kinondoni, Joseph Nicholaus (kushoto), akimtwisha Cecilia Dominic ndoo ya maji baada ya kuzindua mradi wa kisima cha maji katika Kata ya King’ongo, wilayani Kinondoni, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Kisima hicho kimejengwa kwa msaada wa TBL.
Meneja Mauzo wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Kanda ya Kinondoni, Joseph Nicholaus (kushoto), akimtwisha Rehema Mohamed ndoo ya maji baada ya kuzindua mradi wa kisima cha maji katika Kata ya King’ongo, wilayani Kinondoni, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Kisima hicho kimejengwa kwa msaada wa TBL.
Meneja Mauzo wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Kanda ya Kinondoni, Joseph Nicholaus (kushoto), akimtwisha ndoo ya maji mmoja wa akina mama wa Kata hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya MO Resources Ltd, Onesmo Sigalla 9kushoto) akimkabidhi kufuli na funguo pamoja na nyaraka zinginezo za kisima hicho, Meneja Mauzo wa TBL, Kanda ya Kinondoni, Joseph Nicholas ambaye pia alimkabidhi Mwenyekiti Mwenyekiti wa Serikali ya Mataa wa King’ongo, Mapesi (kulia). Kampuni hiyo ndiyo iliyopewa tenda ya kujenga kisima hicho.
Meneja Mauzo wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Kanda ya Kinondoni, Joseph Nicholaus (wa pili kushoto), akipongezwa na mwananchi wa kata hiyo, Abdalah Mangosongo kwa msaada huo wa TBL.
Ofisa Uhusiano wa TBL, Dorris Malulu (kushoto), akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, ambapo alisema kuwa TBL, mwaka huu imetenga sh. mil. 700 kwa ajili ya kuisaidia jamii nchini kuboresha sekta ya maji.
Comments