Sunday, January 10, 2016

WAZIRI NAPE NNAUYE AKUTANA NA WAHARIRI WA VYOMBO VYA HABARI LEO JIJINI DAR

 Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo,Mh.Nnape Nnauye akiwa katika picha ya pamoja na na baadhi ya Wakuu wa Idara ya Habari Maelezo na Wahariri kutoka vyombo mbalimbali vya habari  jana,alipokutana nao na kujadili changamoto mbalimbali zinazoikabiri tasnia hiyo,mkutano huo
umefanyika kwenye moja ya ukumbi ndani ya Uwanja wa Taifa jijini Dar.
  Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo,Mh.Nnape Nnauye akiwa
katika picha ya pamoja na na baadhi ya Wakuu wa Idara ya Habari Maelezo
na Wahariri kutoka vyombo mbalimbali vya habari 
 Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo,Mh.Nnape Nnauye akizungumza na Wahariri wa vyombo vya habari (hawapo pichani), jana jijini Dar,kwenye mkutano uliohusu kujadili mambo mbalimbali zikiwemo changamoto zinazoikabiri tasnia ya habari hapa nchini.Pichani kulia ni Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Absalom Kibanda na kushoto ni  Kaimu Mkurugenzi Idara ya Habari MAELEZO Bi Zamaradi Kawawa . 
 Kaimu Mkurugenzi Idara ya Habari MAELEZO Bi Zamaradi Kawawa akiwakaribisha Wahariri wa vyombo vya habari
(hawapo pichani),jana jijini Dar,kwenye mkutano ulioitishwa na
Waziri Nape kwa ajili ya kujadili mambo mbalimbali yanayoikabiri tasnia
ya habari hapa nchini.Pichani kati ni Waziri Mh.Nape pamoja na
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Absalom Kibanda.

Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Absalom Kibanda akitoa muongozo kwa Wahariri wa Vyombo vya habari (hawapo nchini) kuhusiana na mkutano wao ulioitishwa na Waziri Nape kujadili mambo mbalimbali na changamoto zinazoikabili tasnia hiyo kwa ujumla.
 Baadhi ya Wahariri wa vyombo vya habari wakiwa kwenye mkutano huo wakifuatilia
mambo mbalimbali yaliyokuwa yakijadiliwa ukumbini humo.
 Mmoja wa Wahariri Kulwa Kaledia kutoka New Habari Hause akiomba ufafanuzi wa
jambo kwa Mh Waziri Nape huku baadhi ya wahariri wakifuatilia kwa
makini.
 Mmoja wa Wahariri Grace Hoka akifafanua jambo kwenye mkutano huo
 Baadhi ya Wahariri wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye mkutano huo
 Baadhi ya Wahariri juu pichani wakishiriki kuchangia mambo mbalimbali kwenye mkutano huo.
 Mmoja wa Wahariri akifafanua jambo kwenye mkutano huo
Baadhi ya Wadau wakubwa wa habari pia walikuwepo kwenye mkutano huo .
PICHA NA MICHUZI JR

No comments: