Saturday, January 09, 2016

ASKOFU PENGO APONGEZA HUDUMA ZA TAASISI YA MOYO

Askofu Mkuu wa Jimbo kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana na kupongeza jopo la Madaktari waliomhudumia katika Hospitali ya Mhimbili.
 Katika mkutano huo  Askofu Mkuu wa Jimbo kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo  alitoa zawadi za kadi za pongezi kwa baadhi ya madaktari mara baada ya kuzungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, watoto na Wazee, Ummy Mwalimu akiteta jambo na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Mrisho Kikwete iliyopo katika hospitali ya Taifa ya Mhimbili, Profesa Mohamed Janabi. 

 Askofu Mkuu wa Jimbo kuu la Dar es Salaam Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo akiingia katika ukumbi wa mikutano katika kitengo cha Moyo cha Taasisi ya Jakaya Mrisho Kikwete kilichopo katika Hospitali ya Taifa ya Mhimbili.
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, watoto na Wazee Mhe Ummy Mwalimu akimkaribisha Askofu Mkuu wa Jimbo kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo ili aweze kuzungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
 Kulia ni aliyekuwa Askofu Msaidizi wa Jimbo kuu la Dar es Salaam, Mwashamu Askofu Titus Mdoe na Askofu Mkuu wa Jimbo la Songea, Damian Dallu wakiwa katika mkutano wa Askofu Mkuu wa Jimbo kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo na waandishi wa habari katika ukumbi wa Mkutano wa Kitengo cha Moyo cha Jakaya Mrisho Kikwete iliyopo katika Hospitali ya Taifa ya Mhimbili.

Katibu Mkuu wa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, watoto na Wazee,  Dkt. Mpoki Ulisobisya akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari kuhusiana na swali lililoulizwa na mwandhishi wa habari kuwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, watoto na Wazee haitoi ruhusa ya mtu yoyote kwenda kutibiwa nje ya nchi na ruhusa hiyo hutolewa na Madaktari wenyewe ambao walikua wanamtibia mgonjwa.

Na Chalila Kibuda 
wa Globu ya Jamii.

 Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Katoliki la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo amepongeza weledi wa huduma  za madaktari na huduma zinazotolewa katika Tasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete iliyopo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam.

Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo ametoa pongezi hizo  jana  Ijumaa Januari 8, 2016 wakati akizungumza  na waandishi wa habari hospitalini hapo ambako alikuwa amelazwa kwa uchunguzi wa afya yake na matibabu. 

Alisema kwamba awali yeye alikuwa anaogopa kutibiwa hapo kutokana na taarifa potofu zilizokuwa zinazotolewa kwenye vyombo vya habari juu ya  operesheni tata zilizowahi kufanyika katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili, na kwamba  sasa ameridhika kuwa ni vinginevyo kwani Kitengo cha magonjwa ya moyo cha hospitali hiyo kimemdhihirishia kwamba kina uwezo mkubwa wa matibabu ya moyo kama ilivyo hospitali zingine popote pale duniani.

Askofu Mkuu huyo wa Jimbo kuu la Dar es Salaam Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo alilazwa katika taasisi hiyo ya moyo tangu Januari Mosi mwaka huu. Hali yake imeendelea kuimarika kila siku baada ya kufanyiwa uchunguzi na kupatiwa matibabu hapo.
Kwa upande wake  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, watoto na Wazee, Mhe. Ummy Mwalimu amesema kuwa Serikali imeokoa kiasi cha shilingi bilioni nne ambazo zilikua zipotee kwa ajili ya kupeleka wagonjwa wa moyo kutibiwa  nje ya nchi.
Aidha Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Mrisho Kikwete iliyopo katika hospitali ya Taifa ya Mhimbili, Profesa Mohamed Janabi amesma kuwa Askofu Pengo ataruhusiwa mwisho wa juma hili kwa kuwa afya yake imeimarika.
Post a Comment