Mradi wa Kuwawezesha wanawake kiuchumi kupitia Tasinia ya Urembo ujulikanao kama Manjano Dream Makers hatimaye umefika Mwanza.Wataalamu wa Maswala ya biashara na Urembo Wataendesha Mafunzo Wiki ijayo Traehe 18.01.2016 Kwenye Ukumbi wa Rock city Mall Jijini Mwanza,Wanawake 35 wa jiji la Mwanza Watanufaika na mafunzo ya ujasiriamali kupitia vipodozi vya LuvTouch Manjano.
Wanawake Wakazi wa jiji la Mwanza Wanaopenda Kunufaika na Mradi huo Wanaombwa Kujitokeza Kwa wingi Kujiandikisha siku ya Kesho Tarehe 15.01.2016 kuanzia saa Mbili Asb kwenye Ukumbi wa Rock City Mall .
Mafunzo yana Lengo la kumsaidia mjasiriamali mwanamke kujikwamua. Awamu ya kwanza ni kumfundisha maswala ya Biashara namna ya kuibua na kubuni miradi mbalimbali namna ya kuandika Mpangilio wa Biashara ikiwemo Matumizi sahihi ya Rasilimali Muda, Fedha, Muda na pia namna ya kujitunzia akiba itokanayo na Biashara yake.Baada ya Wanawake hawa kuhitimu Mafunzo haya Taasisi ya Manjano Foundation inatoa Mikopo kwajili ya kuwawezesha Kuanzisha Biashara wakiwa chini ya Uangalizi Maalum wa taasisi hiyo kwa Lengo la Kuhakikisha kila Mhitimu wa Mafunzo haya anapiga hatua na kuweza Kujitegemea .
Wasiliana nasi kwa Simu namba +255 658 741 711 au +255 715 832 420
Comments