Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiongoza mbio za Wabunge Hapa Kazi Tu Dodoma Half Marathon zilizoanzia Bungeni hadi uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma Januari 30, 2016. Kushoyo kwake ni Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye na kushoto ni Naibu Spika wa Bunge, Dkt Tulia Ackson. Mwansasu (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
…………………………………………………………………………………
Na Raymond Mushumbusi MAELEZO.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa,Majaliwa ameyataka mashirikisho ya michezo mbalimbali kumpa mpango kazi wa muda mrefu na mfupi ili kuiwezesha Serikali kushirikiana nao kuleta maendeleo ya michezo nchini.
Mhe.Kassim Majaliwa,Majaliwa ameyasema hayo leo Mijini Dodoma wakati akifunga mashindano ya Hapa Kazi Tu Half Marathon yaliyoanzia katika Chuo cha Biashara (CBE) tawi la Dodoma na kumalizikia katika uwanja wa Jamhuri yenye lengo la kuadhimisha kilele cha Siku 100 za uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt John Pombe Joseph Magufuli tangu aingie madarakani.
“ Serikali ya Awamu ya Tano tumejipanga kuendeleza michezo nchini kwani michezo ni moja kati ya sekta muhimu kwa maendeleo ya wanamichezo na nchi kwaujumla na pia ni moja ya kujitangaza kimataifa kupitia michezo mbalimbali”Alisema Mhe Majaliwa.
Aidha Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Moses Nnauye amesema kupitia wizara yake atajitaidi kuimarisha michezo hasa ukuzingatioa Serikali imeweka mkazo katika michezo hivyo yeye kama waziri mwemye dhamana hiyo atalisimamia kwa karibu suala la maendeleo ya michezo yote .
“Naahidi kushirikiana na vyama vya michezo ili kuimarisha sekta ya michezo kwa kuweka mipango thabiti ya kusimamia na kuiendeleza michezo ili iweze kuleta tjia katika jamii ya watanzania”Alisema Mhe. Nnauye.
Mbio hizi za Hapa Kazi Tu Half Marathon zilmeshirikisha Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt Tulia Ackson,baadhi ya mawaziri, wabunge na watu wa rika zote kwa kukimbia umbali wa kilometa 2, kilometa5 na kilometa21 na washindi kupewa zawadi za pikipiki, mabati na fedha taslimu.
Mashindano haya ya hapa kazi Half Marathon yaliyoandaliwa na Chama cha Riadha Tanzania na kudhaminiwa na kampuni ya GSM, TANAPA, Kilimanjaro International Airport,East Teanders, CRDB Bank na DSTV yameandaliwa kwa nia ya kuandaa timu ya Riadha ya Tanzania kujiandaa na mashindano ya Olompiki yatakayofanyika Rio de Janeiro nchini Brazil.
Comments