Thursday, January 14, 2016

KITWANGA APOKELEWA KWA SHANGWE USAGARA, AMALIZA ZIARA YAKE MISUNGWI, WAMSHUKURU RAIS MAGUFULI KWA KUMTEUA KUWA WAZIRI

NG1
Wananchi wa Kata ya Usagara, wilayani Misungwi wakimshangilia Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Misungwi mkoani Mwanza, Charles Kitwanga wakati alipokuwa akizungumza na wananchi hao katika Viwanja vya Gulio mjini Usagara. Wananchi hao walimwambia Waziri Kitwanga wanaikumbuka ahadi ya Rais John Magufuli wakati akiwa anamnadi Mbunge huyo kipindi cha kampeni, kuwa suala la maji atalishughulikia Rais mwenyewe. Hivyo wanamuomba Mbunge wao ashirikiane na Rais huyo ili maji yaweze kupatikana kwa haraka zaidi. Picha zote na Felix Mwagara.
NG2
Kikundi cha Burudani kinachoitwa Mawe Matatu cha Kata ya Usagara, wilayani Misungwi kikitoa burudani kabla ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Misungwi mkoani Mwanza, Charles Kitwanga (kulia-aliyekaa) kuzungumza na wananchi wa kata hiyo katika Viwanja vya Gulio mjini Usagara. Katika hotuba yake, Waziri Kitwanga aliwashukuru wananchi hao kwa kumchagua na pia atahakikisha kero zote anazitatua. Hata hivyo, wananchi hao,walimwambia Waziri Kitwanga wanaikumbuka ahadi ya Rais John Magufuli wakati akiwa anamnadi Mbunge huyo kipindi cha kampeni, kuwa suala la maji atalishughulikia Rais mwenyewe. Hivyo wanamuomba Mbunge wao ashirikiane na Rais huyo ili maji yaweze kupatikana kwa haraka zaidi.
NG3
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Misungwi mkoani Mwanza, Charles Kitwanga akizungumza na wananchi wa Kata ya Usagara kuhusu masuala mbalimbali ya maendeleo ya jimbo lake. Kitwanga aliwataka wananchi hao washirikiane katika kuchangia miradi ya maendeleo ili jimbo hilo liweze kupata mafanikio zaidi. Hata hivyo, wananchi hao walimuambia Waziri Kitwanga wanaikumbuka ahadi ya Rais John Magufuli wakati akiwa anamnadi Mbunge huyo kipindi cha kampeni, alisema suala la maji atalishughulikia Rais mwenyewe, hivyo wanamuomba Mbunge wao ashirikiane na Rais huyo ili maji yaweze kupatikana kwa haraka zaidi. Hata hivyo maandalizi ya upatikanaji maji zimeanza jimboni humo.
NG4
Msimamizi wa Mradi wa Maji Mwanza, Abbas Muslim akijibu maswali ya wananchi baada ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Misungwi, Charles Kitwanga (kulia) kumtaka ajibu maswali ya wananchi hao kuhusu lini maji yatapatikana jimboni humo pamoja na hatua walizozifikia mpaka sasa. Hata hivyo, Msimamizi huyo alitoa ufafanuazi kuhusu mradi huo na kuwafafanulia wananchi hao kuwa, mradi huo mkubwa wa maji unaojumuisha Misungwi, Magu, Lamadi, Musoma, Bukoba na Jiji la Mwanza unatarajiwa kumalizika mwaka 2018 lakini pia unaweza ukamalizika kabla ya muda huo uliopangwa na wananchi kuweza kupata maji. Picha zote na Felix Mwagara.

No comments: