Wednesday, January 13, 2016

WAZIRI KITWANGA AKABIDHI VITANDA, MAGODORO, MASHUKA JIMBONI KWAKE, AAHIDI KUMALIZA TATIZO LA MAJI NA BARABARA MISUNGWI

kt1
Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya cha Misasi, Ernest Msiba akikijaribu kimoja kati ya vitanda 20 kabla ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Misungwi mkoani Mwanza, Charles Kitwanga (watatu kushoto) kumkabidhi vifaa hivyo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi, Nathan Mshana (wapili kushoto). Waziri Kitwanga alikabidhi vitanda (20), magodoro (20) pamoja na shuka (20) kwa ajili ya Kituo cha Afya cha Misasi pamoja na vitanda sita kati ya hivyo walikabidhiwa Zanahati ya Nyamijundu iliyopo Kata ya Kasololo jimboni humo. Hafla ya makabidhiano hayo ilifanyika katika Kijiji cha Misasi. Kushoto kwa Waziri ni Meneja wa Mfuko wa Pensheni wa PPF Kanda ya Ziwa, Meshack Bandawe, ambapo shirika lake pia lilitoa baadhi ya misaada katika kituo hicho cha afya. Picha zote na Felix Mwagara.
kt2
Meneja wa Mfuko wa Pensheni wa PPF Kanda ya Ziwa, Meshack Bandawe (kushoto) akimkabidhi Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Misungwi mkoani Mwanza, Charles Kitwanga, magaodoro (20) na shuka (20) vyenye thamani ya shilingi milioni tatu na laki tano katika hafla iliyofanyika Viwanja vya Kituo cha Afya Misasi, wilayani Misungwi. Waziri Chikawe baada ya kukabidhiwa vifaa hivyo alivikabidhi kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi, pamoja na vitanda (20) vyenye thamani ya Shilingi milioni 16 ili aweze kuvigawa kwa Kituo cha Afya cha Misasi pamoja na Zahanati ya Nyamijundu iliyopo Kata ya Kasololo jimboni humo.
kt3
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Misungwi mkoani Mwanza, Charles Kitwanga akikata utepe wakati akifungua jiwe la msingi la ujenzi wa Shule ya Msingi ya Ihelele iliyopo Kata ya Ilujamate, jimboni humo wakati alipofanya ziara ya kutembelea miradi ya maendeleo pamoja na kuzungumza na wananchi wa eneo hilo. Waziri Chikawe katika hotuba yake, aliwaahidi wananchi wa eneo hilo upatikanaji wa maji hivi karibuni kwani eneo hilo linamradi mkubwa wa maji wa Mamlaka wa Maji Safi na Usafi wa Mazingira Kahama Shinyanga (KASHWASA), hivyo ni lazima maji yasambazwe kwa vijiji vyote vya jirani.
kt4
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Misungwi mkoani Mwanza, Charles Kitwanga akipanda mti wa kumbukumbu katika eneo la Shule ya Msingi ya Ihelele iliyopo Kata ya Ilujamate, Wilaya ya Misungwi. Shule hiyo inajengwa kwa nguvu ya wananchi pamoja na kuchangiwa na Mamlaka wa Maji Safi na Usafi wa Mazingira Kahama Shinyanga (KASHWASA) ambayo inamradi mkubwa wa maji katika Kijiji cha Ihelele ambapo shule hiyo inapojengwa.
kt5
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Misungwi mkoani Mwanza, Charles Kitwanga akizungumza na wananchi wa Kata ya Misasi mara baada ya kukabidhi vitanda (20), magodoro (20) pamoja na shuka (20) katika Kituo cha Afya cha Misasi wilayani Misungwi. Waziri Chikawe katika hotuba yake aliwaahidi wananchi wa eneo hilo ujenzi wa barabara ya lami pamoja na upatikanaji wa maji.
kt6
Mkuu wa Polisi Wilaya ya Misungwi (OCD), Sylivester Ibrahim akijibu maswali ya wananchi wa Kata ya Misasi kuhusu usalama katika eneo lao. Ofisa huyo wa Polisi alipewa nafasi na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Misungwi mkoani Mwanza, Charles Kitwanga (kulia-aliyekaa) baada ya wananchi hao kutaka kujua masuala ya haki zao waendapo Kituo cha Polisi kuripoti matukio mbalimbali. 
kt7
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Misungwi mkoani Mwanza, Charles Kitwanga akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukabidhi misaada mbalimbali ikiwemo vitanda (20), magodoro (20) pamoja na shuka (20) katika Kituo cha Afya cha Misasi wilayani Misungwi. Picha zote na Felix Mwagara.

No comments: