Thursday, January 21, 2016

SEKRETARIETI YA CHAMA CHA MABUNGE YA JUMUIYA YA MADOLA KANDA YA AFRIKA YAHIMIZA USHIRIKISHWAJI WA WANAWAKE KATIKA NGAZI ZA MAAMUZI.



Mwenyekiti wa Kamati ya Utendaji ya CPA Kanda ya Afrika, Mhe. Lindiwe Maseko (Mb) kutoka Afrika Kusini akiongea na Wajumbe (hawapo pichani) waliohudhuria Warsha ya siku mbili kujadili namna ya kuwashirikisha Wanawake katika ngazi za maamuzi leo jijini Dar es Salaam.

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Utendaji ya CPA Kanda ya Afrika Mbunge toka Afrika Kusini Mhe. Angella Didiza akichangia mada wakati wa Warsha ya siku mbili kujadili namna ya kuwashirikisha Wanawake katika ngazi za maamuzi leo jijini Dar es Salaam.
Katibu Msaidizi Wa Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika kutoka Tanzania, Bwana Demetrius Mgalami akichangia mada wakati wa Warsha ya siku mbili kujadili
namna ya kuwashirikisha Wanawake katika ngazi za maamuzi leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Wajumbe waliohudhuria Ufunguzi wa Warsha ya ya siku mbili ya kujadili namna ya kuwashirikisha Wanawake katika ngazi za maamuzi wakifuatilia hotuba za Viongozi leo jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Kamati ya Utendaji ya CPA Kanda ya
Afrika, Mhe. Lindiwe Maseko (Mb) kutoka Afrika Kusini (aliyekaa katikakati) akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe waliohudhuria Warsha ya siku mbili kujadili namna ya kuwashirikisha Wanawake katika ngazi za maamuzi leo jijini Dar es Salaam.
(Picha zote na Benedict Liwenga)
…………………………………………………………..
Na Benedict Liwenga.
Sekretarieti ya Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika(Commonwealth Parliamentary Association Africa Region
Secretariat
), imefanya Ufunguzi wa Warsha ya siku
mbili inayowakutanisha Wabunge wa Jumuiya ya Madola, Kanda ya Afrika (
Commonwealth Women Parliamentarians Africa Region) kujadili Ushiriki wa Wanawake katika Ngazi za Maamuzi iliyozikutanisha
jumla ya nchi Nane za Afrika.
Akifungua Warsha hiyo leo Jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa
Kamati ya Utendaji ya CPA Kanda ya Afrika, Mhe. Lindiwe Maseko (Mb) kutoka
Afrika Kusini, ameipongeza Tanzania kwa kufanya Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana kwa
amani, uhuru na haki pasipo kumwaga damu na kuwataka nchi nyingine kuiga mfano
huo.
Aidha, Mhe. Maseko ameipongeza Tanzania kwa kuonyesha juhudi
za dhati za kuongeza idadi inayoridhisha ya Wabunge wanawake katika Bunge lake
ikiwa ni sehemu ya kuwashirikisha wanawake katika ngazi mbalimbali za kisiasa
na kijamii
“Licha kutambua majukumu ya mwanamke katika jamii, Warsha hii
hainabudi kujadili masuala ya kuwashirikisha wanawake katika ngazi za maamuzi
na kuongeza idadi yao katika Mabunge na kuwajengea uwezo”, alisema Maseko.
Aliongeza kuwa wanawake ambao wako katika Mabunge hawanabudi
kujiskia huru katika kutekeleza majukumu yao kwani wana haki ya kushiriki
katika masuala yote yakiwemoya kijamii na kisiasa.
Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Utendaji ya
CPA Kanda ya Afrika Mbunge toka Afrika Kusini Mhe. Angella Didiza nae
ameipongeza Tanzania kwa kukubali kufanya warsha hiyo nchini ikiwa ni Makao
Makuu ya Secretarieti na kuongeza kuwa kuna umuhimu wa ushiriki wa wanawake
katika masuala ya ngazi za maamuzi ili kubuni mbinu na mikakati ya kuongeza
idadI ya Wanawake katika ngazi za siasa na kijamii.
Mhe. Didiza ameongeza kuwa, kuna masuala mbalimbali ambayo
yanazihusu nchi ambazo Sekretarieti ya Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola
Kanda ya Afrika licha ya hali ya uchumi kutokuwa nzuri kwa baadhi ya nchi zetu
lakini pia tunanapaswa
 “Masuala ya ulinzi na usalama yana umuhimu wake kwani tumeona matukio mbalimbali yanayohusiana na
manyanyaso ya mwanamke katika masuala ya Uchaguzi na mapigano mbalilmbali
katika baadhi ya nchi lakini pia tumeona jinsi baadhi ya wanawake walivyopoteza
maisha yao wakitetea haki zao wakiwa wagombea”, alisema Didiza.
Aliongeza kuwa Warsha hiyo ni sehemu ya Utekekelezaji wa Mpango wa mafunzo pamoja baina
ya Makao Makuu ya CPA yaliyoko Uingereza na CPA Kanda ya Afrika. Ambapo Dhima
kuu ya Warsha hiyo ikiwa ni “Kuongeza
Ushiriki wa Wanawake
katika Ngazi za Maamuzi”
Kwa upande wake Katibu Msaidizi Wa Chama cha Mabunge ya
Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika kutoka Tanzania, Bwana Demetrius Mgalami
ameeleza kuwa kuwa kufanyikakwa warsha hiyo ni chachu ya maendeleo kwa
kuwashirikisha wanawake katika ngazi mbalimbali za kisiasa na kijamii ambapo
kupitia mada mbalimbali zinazowasilishwa na Wataalam kutoka Tanzania na Kenya ikiwemo
Mifumo ya Uchaguzi ili kuweza kumsaidia mgombea, Sheria na taratibu mbalimbali
ya masuala ya uchaguzi,Sera za Vyama vya Siasa na Akina Mama na Vyombo vya
Habari.
Aidha, nchi zilizoweza kushiriki katika Warsha hiyo ni Tanzania,
Uganda, Kenya, Ghana, Nigeria, Zambia, Mauritus pamoja na Afrika Kusini.
Warsha hiyo inayohudhuriwa na Waheshimiwa Wabunge Wanawake kutoka Mabunge wanachama wa
CPA Kanda ya Afrika inatarajiwa kufungwa siku ya Ijumaa, Januari 22, 2016 na
Spika wa Bunge la Uganda, Mhe. Rebecca Kadaga (Mb), ambae pia ni Mwenyekiti wa
CWP Kimataifa

No comments: