MBUNGE WA JIMBO LA LINDI AENDELEA KUTIMIZA AHADI ZAKE JIMBONI KWAKE

Hassani Selemani Kaunje
Mh. Hassani Selemani Kaunje ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Lindi kupitia chama cha Mapinduzi (CCM) jana aliweza kutekeleza ahadi yake aliyowaahidi kikundi cha wanawake wachuuzi wa samaki cha Mitwero ya kuwapatia msaada wa Majokofu mawili (2) ya kutunzia Samaki.
Akikabidhi majokofu hayo jana Mh. Mbunge amewataka wachuuzi hao kutunza vitu hivyo kwani ni vyagharama na vitadumu kwa muda mrefu endapo wataviweka katika mazingira mazuri. Nao wanakikundi hicho cha akinamama wachuuzi wa samaki wameweza kupongeza hatua hiyo, wamemsifia kuwa ni mtu wa kutimiza ahadi kwani ametimiza kile alicho ahidi.
Hassani KaunjeMh. Mbunge amekuwa mstari wa mbele kutekeleza ahadi zake kwa kipindi hiki kifupi tangu alipochaguliwa na wananchi wa jimbo la Lindi mjini kwani hivi karibuni aliweza kutoa msaada wa Matanki ya kutunzia maji katika kata ya Kineng’ene.

Comments