Friday, January 29, 2016

MCHEKESHAJI KUTOKA KENYA, ERIC OMONDI AWASILI JIJINI DAR ES SALAAM

MWIGIZAJI na mchekeshaji wa nchini Kenya, Eric Omondi amewasili jana mchana  jijini Dar jana akiwa na kikosi kazi chake wakiwa tayari kwa ‘LIVE SHOW’ leo katika ukumbi wa mikutano wa Marqee uliopo hoteli ya Hyatt jijini Dar es Salaam.
Mchekeshaji kutoka nchini Kenya, Eric Omondi akiwa na kikosi kazi chake wakiwasili katika jengo la Alosco Tower lililopo Lumumba jijini Dar es Salaam jana.
Mchekeshaji kutoka nchini Kenya, Eric Omondi akiwa katika pozi na bango la GSM Media jana alipowasili jijini Dar es Salaam kwaajili ya ‘LIVE SHOW’ itakayofanyika kesho katika hoteli ya Hyatt katika ukumbi wa Marqee jijini Dar es Salaam.
Kushoto ni Mchekeshaji kutoka nchini Kenya, Eric Omondi akiwa na Meneja Mkuu wa GSM Media, Deo Ndembeji (katikati) na Dj wa mchekeshaji huo, wakiwa katika ofisi cha GSM Media jana mara baada ya kuwasili jijini Dar es Salaam.
Mchekeshaji kutoka nchini Kenya, Eric Omondi akiteta jambo na Meneja Mkuu wa GSM Media, Deo Ndembeji jana jijini Dar es Salaam.
Kikosi kazi cha Mchekeshaji kutoka nchini Kenya, Eric Omondi.
Meneja Mkuu wa GSM Media, Deo Ndembeji akiwakaribisha wanakikosi kazi wa Mchekeshaji kutoka nchini Kenya, Eric Omondi jana mara baada ya kuwasili katika ofisi za GSM Media zilizopo jengo la Alosco Tower Lumumba jijini Dar es Salaam.
Meneja Mkuu wa GSM Media, Deo Ndembeji na Mchekeshaji kutoka nchini Kenya, Eric Omondi wakiwa katika picha na kikosi kazi cha mchekeshaji huyo ambapo ‘LIVE SHOW’ itakayofanyika leo jijini Dar es Salaam.(Picha na michuziblog)

No comments: