Tuesday, January 19, 2016

MFUKO WA TAIFA WA BIMA YA AFYA KWA KUSHIRIKIANA NA HALMASHAURI YA LINDI VIJIJINI WAZINDUA KAMPENI YA KITAIFA YA UHAMASISHAJI WA CHF KATA YA NYANGAMARA.

if1
Mkurugenzi wa CHF wa NHIF Bw. Mikongoti akikabidhi mashuka 300 yaliyotolewa na NHIF kwa ajili ya vituo vya afya vya Mkoa wa Lindi kwa mkuu wa mkoa wa Lindi Mh. Jordan Rugimbana.
if2
Mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mh. Jordan Rugimbana akikabidhi kadi ya CHF kwa mnufaika mpya wa CHF Bw.  Hassan Namangaya wakati wa Uzinduzi.
if3
Wananchi wa Kata ya Nyangamara wakijitokeza kwa wingi kujisajili na CHF wakati wa uzindizi huo.
if4
Wananchi wa Kata ya Nyangamara wakifuatilia Hotuba ya Mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Lindi.
if5
Mwenyekiti wa CCM wa Lindi Mzee Ali Mtopa alihamasika na kuchangia kaya 8 za wasiojiweza ili waandikishwe kwenye CHF. Alitesimama naye ni Mkuu wa Wilaya ya Lindi Mh. Nawanda.
if6
MKuu wa mkoa Mh. Jordan Rugimbana  akimkabidhi mmoja wa  akina mama ambaye ni mzee kadi ya CHF kama mnufaika mpya wa CHF.
……………………………………………………………………………………….
Mkuu wa Mkoa wa Lindi Bw. Jordan Rugimbana kwa niaba ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Wazee na Watoto amezindua rasmi kampeni ya kitaifa ya uhamasishaji wa Mfuko wa Afya ya Jamii ( CHF) katika kata ya Nyangamara iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Lindi Vijijini.
Katika uzinduzi huo ulioratibiwa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya kwa kushirikiana na Halmashauri ya Lindi Vijijini kaya zipatazo 261(sawa na wanufaika  1,566) zilisajiliwa papo hapo katika CHF kwa mchango wa Shilingi 10,000 kwa mwaka. Pia Mkuu wa Wilaya hiyo Mh. Nawanda alihamasisha viongozi mbalimbali wa Mkoa huo ambao hawakuwepo ambapo zilichangwa fedha kwa ajili ya kaya 2,060 za watu wasio na uwezo ili waandikishwe katika CHF. 
Katika uchangiaji huo Mh. Waziri Mkuu ambaye ni Mbunge wa Ruangwa alichangia usajili wa kaya 900 ambapo  Mkuu wa mkoa wa Lindi Mh. Rugimbana alichangia kaya 100, RAS Lindi – kaya 100, DC Lindi – kaya 50, NHIF kaya 300, Mh. Waziri wa Habari na Mbunge wa Mtama – kaya 300,  Mh. Lalinda Mbunge wa Viti maalum CUF – kaya 50, Mh. Hamida viti maalum CCM – kaya 60, Mh. Hamid Bohali Mbunge wa Mchinga – kaya 100, Mh. Kaunje Mbunge wa Lindi – kaya 100.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa CHF Bw. E. Mikongoti alisema mkoa wa LIndi una wanufaika 89,836 wa CHF ambayo ni asilimia 6.6 ya wana Lindi. Alihimiza Mkoa kuifanya CHF kuwa agenda katika utekelezaji mkoani hapo lakini pia kutumia vema fedha za uchangiaji ili kuboresha huduma za afya ili kuvutia wengi zaidi kujiunga na Mfuko huo. 
Wakati akiwasilisha ripoti ya CHF mkoa wa Lindi, Mganga Mkuu wa mkoa Dk. Sonda alisema Lindi imefanikiwa kupata malipo ya Tele kwa Tele ya CHF ya SHilingi 109,436,000 kwa mwaka 2015 ambazo ni mchangi mkubwa katika kuboresha afya mkoani humo. Hata hivyo aligusia kusema bado wana changamoto ya hamasa ya watendaji kuhusu CHF.
Kwa upande wake Mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Lindi ukizindua uhamasishaji huo aliwahimiza wananchi kuona umuhimu wa kuchangia kiasi kidogo cha fedha kwenye CHF ili wapate kadi ya matibabu kwa kaya kwa mwaka mzima.
Pia alitoa maagizo kwa Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Wilaya za Lindi kuwa kuanzia sasa ni mwisho kufanya matibabu kwa malipo ya papo kwa papo na endapo mtu atalipa papo kwa papo basi alipishwe shilingi 10,000 kila anapoenda kupata matibabu. Alisema haiwezekani kwa mkoa wa Lindi kuwa na asilimia chache hivyo za watu waliojiunga na CHF. Pia alihimiza makundi maalum ya wazee, yatima na wasiojiweza yatafutwe na kuchangiwa fedha ili wajiunge na CHF.
Ali kufanikisha CHF, aliwahimiza wananchi kuwa  huru kuwasilisha malamiko yao kwa uongozi ili yaweze kufanyiwa kazi.
Akikamilisha uzinduzi huo alikabidhi mashuka 300 kwa wakuu wa wilaya yaliyotolewa na NHIF kwa ajili ya vituo vya afya katika mkoa wa Lindi lakini pia alikabidhi kadi za CHF kwa wanachama wapya wa CHF.
Post a Comment