Monday, January 11, 2016

MAALIM SEIF ASEMA HANA TAARIFA JUU YA SWALA LA KURUDIWA KWA UCHAGUZI WA ZANZIBAR

DSC_0068

DSC_0061
Katibu  Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF) na aliyekuwa Mgombea Urais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa tiketi ya Chama hicho, Maalim Seif  Shariff  Hamadi (katikati) akizungumza na waandishi wa habari Januari 11, 2016 katika Hotel ya Serena jijini Dar es Salaam kuhusiana na suala la Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar wa tarehe 25 Oktoba (kushoto), Mwenyekiti wa Mambo ya Siasa wa chama hicho,Twaha Issa, Kulia ni Mshauri wa Mambo ya Siasa wa Chama hicho Bw. Mansour Yusuf.
Maalim Seif  amesema kuwa hana taarifa zozote juu ya swala la  kurudiwa kwa uchaguzi  wa Zanzibar  na badala yake ametaka kura zilizobaki zihesabiwe na mshindi aweze kutangazwa.
Amesema kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jecha Salum Jecha alikuwa hana mamlaka ya kufuta uchaguzi kutokana na hatua zote za uchaguzi.
Amesema kuwa Mwenyekiti wa ZEC hana mamlaka ya kufuta uchaguzi bila kuwa na wajumbe walio wengi wanaounga mkono kile wanachotaka kuamua, hali ambayo haikufanyika wakati wa kufuta uchaguzi huo.
Picha zote na Philemon Solomon-Fullshangweblog.
DSC_0034
Waandishi habari kutoka vyombo mbali mbali vya habari wakiendelea kumsikiliza kwa makini, Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF na Aliekuwa Mgombea Urais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad.
DSC_0044Baadhi ya wapiga picha wa vyombo mbalimbali wakiwa katika mkutano huo uliofanyika kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es salaam leo.

2 comments:

Unknown said...

Ndugu mwenye blog kwanza Fanya editing ya ukurasa huu, hapo ulipoandika kwamba mwenyekiti wa tume ni jaji Mstaafu, jecha hajawahi hata kuwa hata mfyagiaji katika mahakamani, sasa Leo hii unapotosha umma kwa kumuandika kwamba ni jaji mstaafu

Unknown said...

Ndugu mwenye blog kwanza Fanya editing ya ukurasa huu, hapo ulipoandika kwamba mwenyekiti wa tume ni jaji Mstaafu, jecha hajawahi hata kuwa hata mfyagiaji katika mahakamani, sasa Leo hii unapotosha umma kwa kumuandika kwamba ni jaji mstaafu