Kamati ya maadili ya chama cha soka mkoa wa Dar es salaam DRFA ,imewafungia miaka miwili kutojihusisha na masuala ya mpira wa miguu, mwenyekiti wa chama cha soka wilaya ya Temeke Tefa, (Peter Muhinzi),mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi Tefa, (Emanuel Mgaya) na Salim Salehe ambaye ni makamu mwenyekiti wa kwanza na muweka hazina wa TEFA.
Kamati hiyo ya maadili ya Drfa,chini ya mwenyekiti wake,Edward Mwakingwe,imetoa adhabu hiyo baada ya viongozi hao kukaidi maagizo halali ya Drfa ya kutokufanya uchaguzi kulingana na tamko la mwenyekiti wa kamati ya Uchaguzi ya Drfa kutaka uchaguzi huo usifanyike kwakuwa kuna zuio la mahakama.
Mwakingwe asema kitendo cha viongozi hao kukaidi agizo hilo ni kinyume na matakwa ya ibara ya 12 (1) na ibara ya 44 kifungu kidogo cha 4 cha katiba ya Drfa,pamoja na kanuni ya 6 (1) na kanuni namba 9 kifungu kidogo cha pili cha kanuni za nidhamu za TFF.
Hata hivyo wahusika wanayo nafasi ya kukata rufaa kwenye ngazi za juu kama hawataridhika na uamuzi huo.
Comments